Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Bi. Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika
ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana
uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya
Muheza Mkoa wa Tanga.
Ajali hiyo
imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo
hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri
kutoka Tanga kwenda Dar es salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa
likielekea kiwanda cha saruji cha Tanga.
Rais
Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na
amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
"Nimepokea
taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na
naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo" alisema Rais
Magufuli.
Dkt.
Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema pepo, na amewapa pole
majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.
Aidha, Rais
Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo
vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote
zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam.
11 Februari,
2016.
|
Thursday, February 11, 2016
Home
HABARI
MATUKIO
AJALI / PICHA:-Dk. Magufuli Amtumia Salamu Za Rambirambi Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga Kufuatia Ajali Vifo Vya Watu 11.
AJALI / PICHA:-Dk. Magufuli Amtumia Salamu Za Rambirambi Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga Kufuatia Ajali Vifo Vya Watu 11.
Tags
# HABARI
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment