USALAMA WETU:-Tumesherekea kuuona mwaka 2016, Atuko Salama. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, January 02, 2016

USALAMA WETU:-Tumesherekea kuuona mwaka 2016, Atuko Salama.



risasi kova
Baadhi ya siraha zilizokamatwa.

Mwandishi wetu

Matukio ya watu kuporwa pesa kisha kuuawa na majambazi yatikisha, bodaboda zadaiwa kuwa tatizo,licha ya shamrashamra za kusherekea kuuona Mwaka Mpya wa 2016, siyo siri kwamba maisha ya Watanzania hayako salama tena, wameanza kuishi kwa hofu kubwa kufuatia matukio ya mauaji ya raia wema ambayo yamekuwa yakifanywa na majambazi nchini kote kwa kutumia pikipiki na watu kuuawa au kujeruhiwa kwa kupigwa risasi.

 Utafiti uliofanywa  umebaini kwamba, ndani ya muda wa miezi kumi na mbili au mwaka mmoja wa 2015, watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya kwa risasi za majambazi ama wakitoka au kuelekea benki.
IMG-20150420-WA0022
Moja ya tukio la mauaji lililofanywa na majambazi.

Matukio hayo ya kikatili yamewafanya Watanzania kutoa kilio chao kwa serikali wakisema: “Hakuna aliye salama mahali popote, wakati wowote, jeshi la polisi limeshindwa kutulinda.”

Kauli hizo zimetolewa na watu mbalimbali jijini Dar es Salaam, kufuatia tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa Meneja wa Oparesheni wa Kampuni ya huduma za simu ya mkononi ya Zantel, Gabriel Raphael Kamukala aliyepigwa risasi na majambazi akitokea benki maeneo ya Mikocheni, Dar ambapo alitoka ‘kudroo’ shilingi milioni kumi.

Hata hivyo, tukio hilo lilikuja siku chache baada ya Desemba 14, mwaka huu ambapo watu wanne walijeruhiwa vibaya na majambazi waliokuwa na pikipiki kisha kuporwa shilingi milioni nne, jirani na Baa ya Hongera iliyopo Kijitonyama, Dar wakiwa wanatokea benki. 


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad