Rais John
Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman (kulia) uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Uchunguzi
uliofanywa na Nipashe kupitia mahojiano na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya
siasa, uchumi na jamii umebaini kuwa yapo mambo takriban tisa ambayo Watanzania
wengi wanatarajiwa kuyafuatilia kwa karibu ili kujua kitakachotokea.
Kwa kiasi
kikubwa, mambo hayo yamejikita katika Nyanja za siasa, uchumi na kijamii.
Katika
uchunguzi wake, Nipashe imeyabaini mambo hayo kuwa ni utekelezaji wa ahadi ya
elimu bure kwa kila mtoto wa Tanzania kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha
nne; mchuano wa wabunge watokao CCM na wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) vya CHADEMA, Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi; kuendelea kwa mchakato wa katiba mpya; hatma
ya Zanzibar baada ya kufutwa kwa matokeo yake ya uchaguzi mkuu uliofanyika
Oktoba 25,2015; athari za kuendelea kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia;
kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani; tishio
la mvua kubwa za el-nino kwa usalama wa chakula na miundombinu na pia
mustakabali wa utitiri wa magari ya kifahari maarufu kama ‘mashangingi’ katika
taasisi na mashirika ya umma.
“Kuanza kwa
mwaka huu 2016 ni muhimu kwa historia ya Tanzania kwani kuna matumaini makubwa ya
kuanza utekelezaji wa ahadi kubwa za serikali ya awamu ya tano ikiwamo ya
utoaji wa elimu bure, ujenzi wa fly-overs, mpango wa kugawa Sh. milioni 50 kwa
kila kijiji na kila mtaa na pia ujenzi wa zahanati katika kila kijiji,”
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment