Raia Waamilifu, Mathew Charles (kushoto) wa kijiji cha
Kilago na Alphonce Peter toka kijiji cha Ufala wilayani Kahama wakifurahia
jambo walipkuwa wakijadili tatizo la utoro mashuleni
Tukiacha hili
za wazazi kutowapeleka watoto wao shule kwa sababu mbalimbali, ambapo serikali
imekuwa ikiwachulia hatua kali za kisheria wazazi hao, watoto wenyewe nao ni
chanzo cha kingine cha utoro mashuleni.
Wengine wanaaga wamekwenda shule lakini
ukweli ni kwamba hawafiki shule na badala yake wanajificha wanapokujua hadi
muda wa kurudi unapofika nao hurejea majumbani kana kwamba wanatoka shule.
Hivyo ni wajibu
wa raia mwamilifu na aliye mraghbishi anapaswa kuhakikisha watoto wanapata haki
yao hii ya msingi ya elimu. Na hivyo ikibidi hata kutumia nguvu, kama
anavyosimulia Mathew Charles:-“Muda mwingine
nawabeba kwa nguvu watoto hadi shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu.
Nimeshafanya
hivyo kwa watoto watano sasa. Tunajua kwamba wasiposoma sasa watakuwa mizigo
kwenye jamii. Kuna siku watatukumbuka kwamba tulikuwa tunawasaidia,”
Ni dhahiri
kwamba tatizo hili ni kubwa na si jukumu la walimu peke yao?
Kila mwananchi
pale alipo ana jukumu la kuhahakisha huduma bora za jamii zinapatikana kwa
mustakabali wa maendeleo yao. Katika kufanikisha hili raia waamirifu ama
waraghbishi toka katika vijiji vya kata ya Nyandekwa na Kilago wameonesha njia
katika kuhakikisha wanafunzi watoro wanahudhuria shuleni.
|
Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha
Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini.
Akielezea jinsi alivyoamua kushughulikia tatizo hilo
kijijini pao, Paul ambaye pia ni kiongozi wa waraghbishi wapya kutoka kijiji
cha Nyandekwa anasema:
“Nililazimika
kumpigia simu mwalimu mkuu na kuomba kuonana naye kwa lengo la kujadiliana naye
kuhusu hili tatizo. Na pale ndipo nilipoweza kuelewa ukubwa wa tatizo la utoro.
Hivyo nikakubaliana na mwalimu kuwa tutasaidiana katika kuhakikisha kwamba
watoto watoro wanahudhuria shuleni.”
Kwa mujibu wa
orodha aliyokabidhiwa mraghbishi Paul Izengo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Nyandekwa, kuna wanafunzi 21 ambao wameripotiwa utoro kati ya 449 wa shule
hiyo.
Kitendo hiki
cha mraghbishi kuamua pasipo kulazimishwa na mtu kufuatilia suala la utoro wa
wanafunzi katika shule yao ya msingi pale kijijini, ndicho ambacho raia
mwamilifu anatakiwa kukifanya.
Raia mwamilifu
ni yule ambaye anachukua hatua kwa kushirikiana na wanajamii wengine wa maeneo
yake. Huyu ni yule anayetambua majukumu na haki zake kwa mujibu wa ibara ya 12
hadi 24 ya Katiba ya Muungano wa Tanzania.
Huyu ni raia anayependa kuona
mabadiliko chanya kwenye jamii yake. Huyu ni yule anayetenda pasipo
kulazimishwa, bali kwa utashi na uelewa wake kwa mujibu wa sheria na taratibu
zilizowekwa.
Katika
kuhakikisha anaelewa vizuri chanzo cha tatizo hilo, ilimlazimu Paul kwenda
kumtembelea mzazi ambaye mtoto wake yumo kwenye orodha wa watoro. Na huko
alitaka kujua, nini hasa kinachosababisha tatizo hilo.
“Nilikwenda kwa
mama mzazi wa mmoja wa wale watoto walioripotiwa kuwa watoro. Lengo langu
nilitaka kujua nini hasa tatizo mpaka mtoto haendi shuleni. Ndipo nilipogundua
kuna changamoto kubwa zaidi. Inahitajika elimu ya ziada kutolewa,”
Mama mzazi
huyo, alimweleza mraghbishi huyo kwamba michango kwa ajili ya kulipia mitihani
ya watoto wake waliopo darasa la 4 na la 6 ni changamoto kubwa inayomkabili.
Kushindwa huko kuwalipia watoto wake gharama hizo kumepelekea kwa watoto hao
kurudihswa nyumbani.
Sababu nyingine
anayoitaja mama huyo ni upungufu wa chakula hasa watoto wanapokwenda asubuhi na
kurudi shule mchana. Hali hii inasababisha watoto wasiende shule na kujikita
katika shughuli za kuzalisha kwa ajili ya familia.
Pamoja na
changamoto hizo, bado raia huyu mwamilifu alimshauri mama huyo kwenda kuonana
na mwalimu mkuu ili aangalie ni kwa jinsi gani anaweza kusaidiwa ili watoto
wake wahudhurie shuleni.
Ushauri huu
unatokana na ukweli kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo Ramadhani Masatu naye pia
ni raia mwamilifu kwa nafasi yake. Uwamilifu huo unaelezewa na mraghbishi
Elizabeth Ngayalina, toka kijiji cha Nyandekwa:-“Mwalimu mkuu
ni muelewa na ndio maana amekubali kushirikiana nasi. Ametupatia kwanza idadi
ya wanafunzi ambao ni watoro kwa kuwa anajua ni jukumu letu sote si la kwake na
walimu wenzake”
Kwa hakika raia
hawa waamilifu toka katika vijiji vya Nyandekwa na Kilago wanahitaji kuungwa
mkono na wadau wote wa maendeleo. Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto na ndio
maana sera ya serikali ni kutoa bure elimu ya msingi na ile ya sekondari. Njia
pekee ya kumkomboa mtoto ni kumpatia elimu ambayo ndio dira ya maendeleo ya
kila nchi, kuwa na wasomi wengi kadri iwezekanavyo.
CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
No comments:
Post a Comment