Pichani juu na chini ni Mashabiki wa TP Mazembe wakiingia uwanjani kushuhudia fainali hiyo.
Hadi sasa,
Mbwana Ally Samatta na Mtanzania mwenzake anayecheza naye TP Mazembe, Thomas
Ulimwengu wanajivunia rekodi mpya waliyoweka, kuwa Watanzania wa kwanza kucheza
fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na Samatta
anajivunia pia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga bao katika Ligi ya
Mabingwa Afrika- baada ya kufunga bao la pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya
USM Alger katika fainali ya kwanza Jumapili iliyopita mjini Algiers na mchezo
wa leo akifunga la kwanza.
Awali,
Samatta na Ulimwengu walivunja rekodi mbili zilizowekwa na klabu ya Simba SC ya
Dar es Salaam mwaka 1974 na 1993.
1974 Simba
SC iliweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza Nusu Fainali ya
Ligi ya Mabingwa Afrika, walipotolewa na Mehalla El Kubra ya Misri kwa penalti
3-0 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani
kwake.
|
Ukiachana na
rekodi hiyo, Samatta ambaye ni straika wa zamani wa Simba SC ya Tanzania, pia
anawania kutwaa Tuzo ya ufungaji bora Afrika na kuweka rekodi ya kuwa Mtanzania
wa kwanza kufanya hivyo, kwani Kafikisha Mabao Saba na la penati ya leo.
Hii maana
yake huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania inatoa mfungaji bora wa Ligi
ya Mabingwa, baada ya mwaka jana Mrisho Khalfan Ngassa kuongoza pia akiwa na
klabu ya Yanga SC, kabla ya kuhamia Free State Stars ya Afrika Kusini msimu
huu.
Ngassa
alifunga mabao sita sawa na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa
Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.
Baada ya
mchezo huo, Samatta na Ulimwengu watajiunga na kambi ya Taifa Stars huko Afrika
Kusini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Algeri
|
No comments:
Post a Comment