Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John
Pombe Magufuli amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia November 07,2015, hadi hapo maamuzi
mengine yatakapotolewa.
Dk Magufuli
ameagiza shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na
kusimamiwa na mabalozi wanaoiwakilisha
Tanzania nchi za nje.
Uamuzi huo
wa Rais ameutoa Ikulu jijini Dar es Salaam katika kikao kilichojumuisha watendaji mbalimbali
wa serikali wakiwemo Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki
Kuu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu
wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari ruhusa ya safari nje ya nchi inaweza
kutolewa kwa jambo la dharura ambalo hata hivyo jambo hilo lazima lipate kibali
cha Katibu Mkuu Kiongozi.
“Badala yake
rais ametaka ziara nyingi zielekezwe kwenda vijijini ili kuwawezesha watendaji
kujua na kutatua kero za wananchi” imesema taarifa hiyo.
Katika kikao
hicho, rais ameelekeza pia mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa
kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili yasimamiwe mara moja na
Baraza la Mawaziri atakaloliteua.
Mambo hayo
ni pamoja na kuanza kwa mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza
kupatiwa elimu ya bure kuanzia Januari mwakani,2016.
Taarifa hiyo
imetaja jambo la pili kuwa ni suala la uratibu wa mikopo ya wanafunzi wa elimu
ya juu ambapo ameagiza lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya
utekelezaji mzuri zaidi.
Kwa mujibu
wa taarifa hiyo, rais amemuagiza Kamishna wa TRA kusimamia kwa makini zoezi la
ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kero ndogo ndogo zinazowakabili wananchi
zinaanza kushughulikiwa mara moja.
Ameitaka TRA
kukusanya mapato toka kwa wafanya biashara wakubwa na wakwepa kodi bila kuogopa
mtu wala taasisi yoyote na kusisitiza kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kubatilisha
maamuzi hayo zaidi yake.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Sunday, November 08, 2015
HAPA KAZI TU:-Rais Maguful afuta Safari zote za nje ya Nchi kuanzia November 07,2015.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment