Waandishi wa
habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Msitafu
Damian Lubuva .
Na Chalila
Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Viti Maalum vya Wabunge 110 kwa vyama vitatu
ambavyo vimevuka asilimia tano ya kura za wabunge.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu,
Damian Lubuva amesema idadi ya wabunge imeongezeka kwa kufikia asilimia 40
kutokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 kwa kuongeza idadi ya viti maalum
vya wanawake.
Lubuva
amesema kutokana na kuwepo majimbo ya nane ambayo hayakufanya uchaguzi
kunafanya viti vitatu kutokuwepo, baada ya uchaguzi wa majimbo hayo viti
vitarudi kwa vyama.
Katika
mgawanyo wa viti maalumu vya wanawake katika bunge linalotarajiwa kuanza hivi karibuni Chama cha
Mapinduzi (CCM), kimepata viti 64, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
viti maalum 36 na Chama cha Wananchi (CUF)
Viti Maalum 10.
Majina ya
viti maalum yatapatikana katika vyama
husika kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa
Tume ya kila chama ili tume iweze
kufanya uteuzi.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, November 06, 2015
BUNGE LA TANZANIA:- Huu ndio Mgawanyo wa Viti Maalumu 110 kwa CCM,CHADEMA na CUF.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment