Mashabiki
wakishangilia ushindi wa timu yao... Simba SC imepata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya
Kagera Sugar.
|
Mashabiki wa
timu ya Simba wakizawadia fedha mshambuliaji wa timu hiyo Hamisi Kiiza
aliyefunga magoli matatu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kuwa HAT TRICK
ya kwanza ya msimu huu 2015/2016 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
|
Pichani ni Hamisi Kiiza
akipokea zawadi ya fedha na kofia kutoka kwa mashabiki wa timu ya Simba SC
ambapo Baada ya mpira kumalizika baadhi ya mashabiki walioukuwa wamekaa karibu
na lango kuu la kuingilia na kutokea uwanjani, walimwita mshambuliaji huyo
aliyetupia hat-trick ya kwanza msimu huu na kumpa zawadi za pesa na vitu
vingine kutokana na kufurahishwa na kiwango alichokionesha Kiiza.
|
Kiiza
hakusita kupokea fedha hizo kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiimba wimbo wa
kumsifia Kiiza wakati akitoka uwanjani. Baada ya kuzipokea zawadi hizo Kiiza
aliwashukuru mashabiki hao na kuelekea vyumbani…PICHA KWA HISANI YA SHAFFIH DAUDA.
Ligi kuu
Vodacom Tanzania bara 2015/2016, iliendelea jana September 20,2015 kwa michezo mitano kupigwa
kwenye viwanja vitano tofauti, ukiachana na mchezo kati ya Simba SC dhidi ya
Kagera Sugar uliomalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 3-1 kwenye
uwanja wa Taifa matokeo mengine yalikuwa kama ifuatavyo.
Azam FC
imeendeleza ushindi na kuendelea kukimbizana na Simba SC na Yanga SC baada ya
kuifunga timu ya Mwadui FC kwa goli 1-0 mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa
Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Bao pekee
kwenye mchezo huo limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’.
Agrey Morris
alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mwadui kuzawadiwa penati lakini mshambuliaji
wa Mwadui Rashid Mandawa alishindwa kukwamisha wavuni mkwaju huo wa penati.
Kwenye
uwanja wa Manungu mjini Morogoro, Mtibwa Sugar walikuwa wenyeji wa Ndanda FC na
Mtibwa imefanikiwa kushinda kwa goli 2-1 dhidi ya Ndanda FC.
Magoli ya
Mtibwa yamefungwa na Salim Mbonde dakika ya kipindi cha kwanza na Said Bahanuzi
akafunga goli la pili kwa upande wa Mtibwa Sugar huku goli pekee la Ndanda
likifungwa na Kigi Makasi.
Mchezo kati
ya Coastal Union dhidi ya Toto Africans umemalizika kwa timu hizo kutoka sare
ya kutofungana kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
MATOKEO VPL
2015/2016.
Jumamosi
Septemba 19,2015.
Yanga SC 4 – 1
JKT Ruvu 1
Stand United
2 – 0 African Sports
Mgambo
Shooting 1 – 0 Majimaji
Tanzania
Prisons 1 – 0 Mbeya City
RATIBA MECHI
ZIJAZO
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment