KAMPENI UKAWA 2015:- Nembo ya M4C iliyobadilishwa , Chadema kumburuza Dk. Magufuli Mahakamani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 19, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:- Nembo ya M4C iliyobadilishwa , Chadema kumburuza Dk. Magufuli Mahakamani.


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kumshitaki mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli kwa madai ya kutumia vibaya nembo za chama hicho.

    Ni baada ya Dk. Magufuli kutangaza kuwa nembo ya Movement for Change (M4C) ‘kuipora’ wakati akifanya mkutano wake wa kampeni mkoani Kigoma kwenye Uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji.

 Katika mkutano huo Dk. Magufuli alisema “hawa jamaa zangu wa Chadema wananipenda, hata ile nembo yao ya M4C ni Magufuli for Change-maana yake Magufuli kwa Mabadiliko.

Chadema wanaratajia kufungua kesi hiyo Septemba 21 mwaka huu,2015 na kwamba, madai hayo yatakwenda sambamba na madai ya kutumia kauli mbiu ya ‘mabadiliko Lowassa’ ambayo kaibadilisha na kuwa ‘mabadiliko Magufuli’.
.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana September 18,2015, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ngome Kawe, Mwanasheria wa Chadema, John Malya amesema “CCM imekuwa ikivunja sheria za uchaguzi kila siku bila kuchukuliwa hatua yoyote na mamlaka husika, wanatumia nembo za Chadema ambazo zimesajiliwa na kujulikana.”

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari..’Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa hususani mambo ya kisheria yanayoendelea kwenye kampeni zoezi la uchaguzi ni zoezi la kikatiba, sheria ya uchaguzi wa taifa mwaka 1985 kanuni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na maadili ya uchaguzi wa Ubunge, Urais na Udiwani pamoja na sheria nyingine ikiwemo ya rushwa na sheria ya vyama vya kisiasa – John Mallya..

.

Sheria kwa mfano ambayo ni maadili ya Uchaguzi ya mwaka huu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu kupitia makatibu wake wakuu  wameweka sign zao inakataza kwa mfano suala la mtu kutoa bango la mtu mwingine lakini chadema imepata hiyo changamoto kwamba mabango yake wameondolewa kwa mfano hili bango lipo Nyerere Road pale Mwanza limeondolewa na watu wa CCM ilikuwa ni nyumbani ya mtu binafsi wakamtishia watachoma nyumbani yake wakamrushia mawe wakavunja vioo vyake na baada wakaliondoa‘ – John Mallya..

.

Na hii inaonesha sio tu ni namna gani CCM sio tu wamekiuka sheria lakini hawafai kutawala nchi  kwasababu suala la kuweka bango ni suala la kisheria ukiona bango la Samia,Magufuli na mtu yoyote limewekwa kisheria‘ – John Mallya

.

‘Mabango, sera, vipeperushi vyote vinakuwa vimesajili na tume ya Uchaguzi kwa madhumuni ya Kampeni kwa mfano ujumbe wa Mabadiliko umesajiliwa na nembo ya CHADEMA pia imesajiliwa,  sasa CCM wanakiuka sheria wame ku copy na ku paste wanachukua ilani na sera zetu ambapo wamechukua nembo yetu M4C ambayo sisi tunaita Movement 4 Change huku CCM wakiwa wanasema M4C ni Magufuli 4 Change‘ – John Mallya.
.

Waandishi wa Habari./Habari kwa hisani ya Millardayo.

Katika hili tumechukua hatua nzito kuliko hizi za mwanza maana yake hili sio la kimadili hili ni uvunjwaji wa sheria,  Chadema tunampeleka Magufuli Mahakamani  pamoja na bodi ya wadhamini wa chama cha Mapinduzi‘ – John Mallya

Unaweza uka bonyeza HAPA kumsikiliza John Mallya.


 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad