KAMPENI UKAWA 2015:-Lowassa Asimikwa Kuwa Chifu Wanyaturu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 15, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:-Lowassa Asimikwa Kuwa Chifu Wanyaturu.



Mmoja wa wazee wa Kimila wa Kabila la Wanyaturu, Mzee Semani Nyambia akimvisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, vazi la kimila (mgololi) ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa mlezi wa Wanyaturu, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini,
Mmoja wa wazee wa Kimila wa Kabila la Wanyaturu, Mzee Semani Nyambia akimvisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, vazi la kimila (mgololi) ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa mlezi wa Wanyaturu, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini.

 


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, Septemba 13, 2015. 

Katika hotuba yake, Lowassa amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi kuwa Rais wa Tanzania, ataanzisha viwanda vya kusindika zao la alizeti, ili wakulima wa zao hilo waweze kufaidika na pia atakabiliana na kero zote za Mkoa wa Singida kwa ujumla. Lowassa, Jana  Septemba 14, 2015 ataendelea na ziara yake ya Kampeni katika Mkoa Shinyanga, baada ya kumaliza katika Mkoa wa Singinda, kwenye Majimbo ya Manyoni Magharibi, Singida Kaskazini, Iramba Mashariki na Iramba Magharibi.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA katika Jimbo la Singida Kaskazini, David Djumbe,  wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, Septemba 13, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, baadhi ya wagombea wa Udiwani wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ilongero, Jimbo la Singida Kaskazini, Septemba 13, 2015.



Wananchi wa Ilongero, Singida Kaskazini wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa.


Wakiperuzi picha za Mgombea wao.
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad