FA CUP:-Hii ndio droo ya nusu fainali Arsenal kuwavaa Bradford or Reading huku Aston Villa uso na Liverpool or Blackburn at Wembley. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 10, 2015

FA CUP:-Hii ndio droo ya nusu fainali Arsenal kuwavaa Bradford or Reading huku Aston Villa uso na Liverpool or Blackburn at Wembley.

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Arsenal imetinga nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuitandika Manchester united magoli 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford usiku wa jana March 09,2015.

 Mchezaji wa zamani wa Man United Danny Welbeck aliifungia Arsenal bao la ushindi katika dakika ya 61.

Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao Nacho Monreal na baadaye Man United kusawazisha dakika ya 29 kupitia kwa nahodha wao Wayne Rooney kabla ya Welbeck kuhitimisha ushindi.



Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada ya Angel Di Maria kulambwa Kadi za Njano mbili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Huu ulikuwa ni Usiku mwema kwa Arsenal na Mashabiki wake ambao wameendelea kutetea vyema Kombe la FA CUP ambalo wao ni Mabingwa Watetezi na pia wamekuwa wakiteswa na Man United kwa kufungwa Mechi 11 kati ya 15 zilizopita.



Pia kwenye Droo ya Nusu Fainali ya FA CUP, iliyofanyika mara baada ya Mechi hiyo, Arsenal watacheza na Mshindi kati ya Bradford City au Reading ambao Jumamosi March 07,2015, walitoka 0-0 kwenye Mechi yao ya Robo Fainali.

Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya Mshindi wa Liverpool na Blackburn Rovers, ambao nao walitoka 0-0, dhidi ya Aston Villa.


FA CUP RATIBA / MATOKEO - ROBO FAINALI.

Jumamosi Machi 7,2015.

Bradford 0 - 0 Reading  

Aston Villa 2 - 0  West Brom 

Jumapili Machi 8,2015.

Liverpool 0  - 0 Blackburn 
            
Jumatatu Machi 9,2015.

Man United 1 - 2  Arsenal 
    
TAREHE ZA RAUNDI.

-Raundi ya 6 [Robo Fainali]: 7 Machi 2015.

-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015

-Fainali: 30 Mei 2015.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad