IDRIS:- Nafikiria Maisha ya Baadaye…Si hela Nilizopata. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 12, 2014

IDRIS:- Nafikiria Maisha ya Baadaye…Si hela Nilizopata.

Mshindi wa Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan, akiwa kwenye pozi.

Meneja Uhusiano wa Multchoice Barbara Kambogi (kushoto),akiwa na  Idrisa (katikati) na Meneja  Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu,  katika meza kuu.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye tukio hilo.

Mshindi wa Big Brother Hotshots, Mtanzania  Idris Sultan, hivi sasa anafikiria zaidi maisha yake ya baadaye badala ya kufikiria fedha alizopata katika shindano hilo lililomalizika hivi karibuni Afrika Kusini.

Alisisitiza kuwa ataendelea kuwasaidia vijana walio katika changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga vita madawa ya kulevya, mimba za utotoni na mengineyo.

Hayo ameyasema Jana Desemba 11,2014, jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili jana  kutoka Afrika ya Kusini na kulakiwa na Watanzania katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na maofisa wa kampuni ya Multchoice Tanzania.

Akizungumza pia katika hafla hiyo, Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi, amesema Idris atakuwa chini ya kampuni hiyo kwa miezi kadhaa na kufanya naye kazi katika miradi mbalimbali.

 Idris alitoa shukrani nyingi kwa Watanzania  na Waafrika kwa ujumla kwa kumpigia kura iliyomwezesha kushinda kitita Dola 300,000 za Marekani.Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com

(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad