SOKA 2013/2014:-Manchester City Mabingwa watarajiwa Jumapili-Mei 11,2014-Etihadi huku Real Madrid Ubingwa ukiota mbawa La Liga. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Thursday, May 08, 2014

demo-image

SOKA 2013/2014:-Manchester City Mabingwa watarajiwa Jumapili-Mei 11,2014-Etihadi huku Real Madrid Ubingwa ukiota mbawa La Liga.

.com/simgad/
Screen-Shot-2014-05-07-at-11.43.57-PM

Ni mchezo wa Ligi Manchester City ikishinda magoli 4-0 dhidi ya Aston Villa- magoli ambayo yamefungwa na Dzeko kwenye dakika 64′+ 72′+ Jovetic 89′ + Yaya Toure kwenye 90 +3) na kwa mara ya 25 Msimu huu, uongozi wa Ligi Kuu Uingereza ukibadilika Usiku wa Mei 07,2014, Uwanjani Etihad uliokumbwa na Mvua kali baada ya Manchester City kushinda ushindi huo na kuipiku Liverpool kileleni na sasa wako Pointi 2 mbele huku kila Timu ikiwa  imebakiza Mechi moja tu.

Screen-Shot-2014-05-07-at-11.44.49-PM

Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2013/2014 unamalizika Jumapili Mei 11,2014 kwa Man City kucheza Nyumbani na West Ham na wanahitaji Pointi 1 tu kutwaa Ubingwa huku labda Liverpool washinde na Man City wakitoka Sare, na kufuta Tofauti ya Mabao 13 ya Man City au  Man City wafungwe Mechi hiyo na Liverpool kushinda….Mechi ya jana (Mei 07,2014) pia imefuta kabisa matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa.

1399490156286_lc_galleryImage_Manchester_City_s_Vincent

Nafasi pekee na safi waliyopata  Aston Villa ya kufunga ni pale Kichwa cha Weimann kugonga Posti ya Juu na kudunda chini nje ya Mstari wa Goli na kumwacha Mshambuliaji huyo asiamini nini kimetokea.

1399489050826_lc_galleryImage_Manchester_City_s_Belgian

1399492615640_lc_galleryImage_MANCHESTER_ENGLAND_MAY_07

1399494233831_lc_galleryImage_epa04195720_Manchester_Ci

Nao :-Sunderland walishinda bao 2-0 dhidi ya West Brom kwa bao za Colback, Dakika ya 13 na Borini dakika ya 31 na kujihakikishia kabisa kubaki Ligi Kuu Uingereza msimu ujao.

Mechi za Mwisho za Msimu Ligi kuu Uingereza 2013/2014

Jumapili 11 Mei 2014.



[Mechi zote Saa 1100 Jioni, Saa za Bongo]

Cardiff v Chelsea

Fulham v Crystal Palace

Hull v Everton

Liverpool v Newcastle

Man City v West Ham

Norwich v Arsenal

Southampton v Man United

Sunderland v Swansea

Tottenham v Aston Villa

West Brom v Stoke

Screen-Shot-2014-05-07-at-11.43.42-PM

Liverpool ndiyo timu nyingine yenye nafasi ya kutwaa ubingwa kama itashinda mechi ya mwisho dhidi ya Newcastle na City wapoteze dhidi ya West Ham.


Katika Mchezo wa Ligi ya Hispania Jana usiku-Mei 07,2014:-Matumaini ya Real Madrid kutwaa taji la La liga yalifanywa kuwa magumu baada ya kulazimishwa kutoka sare ya kufungana boa 1-1 na Real Valladolid katika mchezo wa ugenii.

lilikuwa ni boa la Humberto Osorio dakika ya 85 lililoipokonya tonge mdomoni timu ya Kocha Carlo Ancelotti, baada ya beki Sergio Ramos kufunga kwa staili ya mipira ya adhabu ya Cristiano Ronaldo kuipa Real Madrid bao la kuongoza dakika ya 35.


article-0-1DA687B000000578-115_634x479

Real Madrid sasa imefikisha pointi 84 baada ya kucheza mechi 36 na kubaki nafasi ya 3 nyuma ya FC Barcelona yenye pointi 85 ,mechi 36, wakati Atletico Madird wanaendelea kula raha kileleni kwa pointi zao 88 za mechi 36 pia na Mechi zimebaki 2 tu.


MECHI ZILIZOBAKI LA LIGA 2013/2014.

ATLETICO MADRID

-Mei 11,2014: Atletico v Malaga

-Mei 18,2014: Barcelona v Atletico

REAL MADRID

-Mei 11,2014:Celta Vigo v Real

-Mei 18,2014: Real v Espanyol

FC BARCELONA

-Mei 11,2014: Elche v Barca

-Mei 18,2014: Barca v Atletico


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *