Tazama Taswira ya Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dr. Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na Mvua. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 06, 2013

Tazama Taswira ya Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dr. Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na Mvua.

Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.
Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo (Desemba 06,2013) ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope.
Gari ikiwa imekwishaondolewa kwenye eneo korofi tayari kwa kuendelea na msafara kutoka Wilaya ya Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,ItIkadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro amemaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.
 Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad