Tazama matokeo ya Darasa la Saba 2013……..hapa……….! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 29, 2013

Tazama matokeo ya Darasa la Saba 2013……..hapa……….!


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini akitangaza wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga  kidato cha kwanza 2014, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, Dar es Salam ... Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Zuberi Samataba..huku  katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili.


Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza  mwakani  kutokana na matokeo ya darasa la saba  ambapo wanafunzi  427,609 kati ya  844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika.

Jumla ya wanafunzi  844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad