SOMA:-Droo UEFA ya Raundi ya mtoano ya Timu 16 inavyowezakuwa Jumatatu Desemba 16,2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 12, 2013

SOMA:-Droo UEFA ya Raundi ya mtoano ya Timu 16 inavyowezakuwa Jumatatu Desemba 16,2013.



Timu zote zinatazamiwa kutoepuka kukutana na vigogo wa Hispania, Real Madrid na FC Barcelona, wakati timu ya Arsene Wenger inaweza kukutana na mabingwa watetezi, Bayern Munich - City haiwezi kukutana na Bayern lakini inaweza kukutana na washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund.

Anapambana kuwa fiti: Lionel Messi atarajea kutoka kwenye majeruhi kuiongoza Barcelona katika hatua ya mtoano huku mwenzake Cristiano Ronaldo atataka kuboresha rekodi yake ya mabao aliyoanza nayo katika hatua ya makundi akiwa Real Madrid.
DROO ya UEFA CHAMPIONZ  LIGI, ili kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itafanyika huko Nyon, Uswisi Jumatatu Desemba 16 kuanzia Saa 8 Mchana.

Katika Droo hiyo, Mabingwa Watetezi, Bayern Munich na Washindi wa Pili, Borussia Dortmund, wamo pamoja na wenzao wengine wawili wa Germany, Bayer Leverkusen na FC Schalke.

Ligi Kuu England inazo Timu 4 ambazo ni Mabingwa wake Manchester United, Man City, Chelsea na Arsenal.

Real Madrid, ambao wanasaka Taji lao la 10 Ulaya, wamo pamoja wenzao wa Spain, Barcelona na Atletico Madrid.

Italy imebakiwa na Timu moja tu ambayo ni AC Milan.

Miongoni mwa Timu hizo 16 ambazo zimo kwenye Droo, 4 zimetokea kwenye Raundi za Awali za Mchujo za UCL Msimu huu.

Kwa mujibu wa Kanuni za Droo, Timu zitawekwa kwenye Vyungu viwili, Chungu Namba 1 ni wale Washindi wa Makundi na Chungu Namba 2 ni Washindi wa Pili wa Makundi.

CHUNGU NA 1-WASHINDI WA MAKUNDI.

-Manchester United FC (England)
-Real Madrid CF (Spain)
-Paris Saint-Germain (France)
-FC Bayern München (Germany, Mabingwa Watetezi)
-Chelsea FC (England)
-Borussia Dortmund (Germany)
-Club Atlético de Madrid (Spain)
FC Barcelona (Spain)

CHUNGU NA 1-WASHINDI WA PILI WA MAKUNDI.
 
-Bayer 04 Leverkusen (Germany)
-Galatasaray AÅž (Turkey)
-Olympiacos FC (Greece)
-Manchester City FC (England)
-FC Schalke 04 (Germany)
-Arsenal FC (England)
-FC Zenit (Russia)
-AC Milan (Italy)

Droo hii itaendeshwa na Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi wa Mashindano wa UEFA, Giorgio Marchetti, wakisaidiwa na Balozi wa Fainali za UCL 2013/14, Gwiji Luis Figo.

Kitakacho zingatiwa ni kuwa Timu toka Chungu Namba 1 itapambanishwa na Timu toka Chungu Namba 2 isipokuwa Timu zilizotoka Kundi moja au Nchi moja hazitaruhusiwa kukutana.

Pia, Washindi wa Makundi wataanza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 Ugenini hapo Februari 18/19 na 25/26 na kumalizia Nyumbani hapo Machi 11/12 na 18/19.

UCHAMBUZI KWA TIMU 16 na WASHINDI WA MAKUNDI.

KUNDI A: Manchester United 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Schalke, Zenit, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa wa England

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Wayne Rooney, Antonio Valencia Bao 2
MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Mtoano Timu 16

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 3 (1968, 1999, 2008)

KUNDI B: Real Madrid 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit, Milan.

WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili Spain

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Cristiano Ronaldo Bao 9

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Nusu Fainali

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 9 (1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002)

KUNDI C: Paris Saint-Germain 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, France

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Zlatan Ibrahimović Bao 8

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Robo Fainali

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali (1995)

KUNDI D:  FC Bayern München 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Arsenal, Zenit, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa Watetezi

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Mario Götze, Thomas Müller, Franck Ribéry, Arjen Robben Bao 3

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Mabingwa (2-1 v Borussia Dortmund, Wembley)

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 5 (1974, 1975, 1976, 2001, 2013)

KUNDI E: Chelsea FC 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Zenit, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Mshindi wa Tatu, England

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Demba Ba, Samuel Eto'o, Ramires, Fernando Torres Bao 2

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi, baadae Europa League Mabingwa

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa (2012)

KUNDI F: Borussia Dortmund 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Zenit, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili, Germany

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Robert Lewandowski Bao 4

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Fainali (1-2 v FC Bayern München, Wembley)

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa (1997)

KUNDI G: Club Atlético de Madrid (ESP)

WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Milan

WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Tatu, Spain

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Diego Costa 4

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: UEFA Europa Ligi Raundi ya Timu 32

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (1974)

KUNDI H: FC Barcelona 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Leverkusen, Galatasaray, Olympiacos, Manchester City, Schalke, Arsenal, Zenit

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Spain

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Lionel Messi Bao 6

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: semi-finals

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwa x 4 (1992, 2006, 2009, 2011)

WASHINDI WA PILI WA MAKUNDI.

KUNDI A: Bayer 04 Leverkusen 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Paris, Chelsea, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Tatu, Germany

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Simon Rolfes Bao 3

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: UEFA Europa Ligi Raundi ya Timu 32

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (2002)

KUNDI B: Galatasaray AÅž 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Turkey

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Umut Bulut Bao 3

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Robo Fainali

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali (1989)

KUNDI C: Olympiacos FC (GRE)

WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Mabingwa, Greece

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Kostas Mitroglou Bao 3

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi baadae Europa Ligi Raundi ya Timu 32

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Robo Fainali (1999)

KUNDI D: Manchester City FC 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Bayern, Paris, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Washindi wa Pili, England

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Sergio Agüero Bao 6

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Makundi

KUNDI E: FC Schalke 04 (GER)

WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya 4, Germany

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Julien Draxler Bao 3

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Nusu Fainali

KUNDI F: Arsenal FC 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Real Madrid, Paris, Bayern, Atlético, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya 4, England

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Olivier Giroud, Aaron Ramsey, Jack Wilshere 2

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Washindi wa Pili (2006)

KUNDI G: FC Zenit 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Barcelona

WAMEINGIA UCL KAMA: Mshindi wa Pili, Russia

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Hulk, Aleksandr Kerzhakov Bao 2

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Makundi baadae Europa Ligi Raundi ya Timu 16

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Raundi ya Timu 16

KUNDI H: AC Milan 

WANAWEZA KUKUTANA NA: Manchester United, Real Madrid, Paris, Bayern, Chelsea, Dortmund, Atlético

WAMEINGIA UCL KAMA: Nafasi ya Tatu, Italy

MFUNGAJI BORA HATUA YA MAKUNDI: Mario Balotelli Bao 2

MSIMU ULIOPITA HATUA WALIYOFIKIA: Raundi ya Timu 16

MAFANIKIO MAKUBWA MASHINDANO YALIYOPITA: Mabingwas x 7 (1963, 1969, 1989, 1990, 1994, 2003, 2007)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad