Mwili
ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye
jengo la Muungano.
Msafara
wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi
siku ya jumatano.
Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya
Afrika Kusini.
Wananchi
walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa
heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara
ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa
askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's Joseph Winter katika mji wa Pretoria
amesema.
Wanajeshi
waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano
eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Wanachi,
wakuu wa nchi walioalikwa na wageni wengine wa kimataifa watapata nafasi ya
kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu aliyefariki alhamisi akiwa na
umri wa miaka 95.
Wageni hata
hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Leo jioni
wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la
kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.
Marehemu
Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape
Mashariki siku ya jumapili.
Maelfu ya
raia wa Afrika ya kusini hapa jana waliungana na viongozi mbali mbali duniani
katika ibada ya kumbu kumbu siku ya jumanne kama sehemu ya mfululizo wa
maombolezo kifo chicho.
No comments:
Post a Comment