Breaking News:-Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kibondo kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 06, 2013

Breaking News:-Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kibondo kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba.


Ziara ya Dr Wilbroad Slaa Mkoani Kigoma iliyoanzia katika wilaya ya Kakonko( Dec 05 na itamalizika Dec 15,2013) inafanyika siku chache baada ya Chadema Mkoani humo kupendekeza iahirishwe kwa madai kuwa usalama sio shwari katika baadhi ya majimbo na kisha kutangaza tena kuwepo kwa ziara hiyo.


Jeshi la Polisi wilayani Kibondo mkoani Kigoma limewakamata watu wanne kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo

Mwandishi wa Redio Kwizera Fm James Jovin amesema kuwa watu hao walikuwa na mabango yenye maneno yanayoonesha kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ya kuwavua madaraka Zitto Kabwe na wenzake, lakini hata hivyo wameelekezwa sehemu ya kukaa ili mabango yao yaweze kusomwa vizuri na Dk Slaa, wamekaidi malelekezo hayo ambapo imebidi Dk Slaa aliagize jeshi la Polisi kuwakamata watu hao kwani mkutano huo ni kwa mujibu wa sheria

Watu hao ambao majina yao hayakujilikana papo hapo wamepelekwa kituo cha Polisi na Dk Slaa amemuagiza Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kibondo kufuatilia kesi hiyo kwa ukaribu

ZAIDI SOMA HAPA:- https://www.facebook.com/radiokwizera/posts/585381244851094?notif_t=like

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad