Watu sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 04, 2013

Watu sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya.


Gari la Abiria aina ya Hiace likiwa limegongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Land Cruiser katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya Jana (Juni 03,2013) huku Watu sita wakifariki Dunia papo Hapo na wengine Sita kujeruhiwa.


Gari la Abiria aina ya Hiace likiwa limegongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Land Cruiser katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya Jana (Juni 03,2013) huku Watu sita wakifariki Dunia papo Hapo na wengine Sita kujeruhiwa.


Baadhi ya Miili ya maiti iliyookolewa baada ya ajali kutokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya Jana (Juni 03,2013) .



Baadhi ya  Wananchi mbalimbali  wakiwa katika eneo la tukio kushuhudia  ajali iliyotokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mkoani Mbeya Jana (Juni 03,2013) huku Watu sita wakifariki Dunia papo Hapo na wengine Sita kujeruhiwa.


Watu 6 wamefariki Dunia na wengine 6 kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyotokea Nanenane Darajani eneo la Uyole mkoani Mbeya.




Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na Dereva mmoja wa Hiace. 




Kamanda Barakael Masaki.
Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T 178 AAV aina ya Toyota Hiace iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya  Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea Uyole.




Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano zaidi.




Maiti nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.




Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake watano na Mwanamke mmoja ,ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.




Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni  mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. 



Picha na Mbeya yetu Blog.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad