![]() |
Ndugu Hamis Salum baba wa mtoto ambaye Quran yake imekojolewa.
|
Mji wa MBAGALA na vitongoji vyake Jijini Dar es
Salaam umekumbwa na fujo, vurugu na
visasi baada ya mtoto wa kiume anayedaiwa kusoma kidato cha pili kukojolea
kitabu kitakatifu cha QURUAN.
Vurugu hizo zimetokea
eneo la Mbagala Kizuiani ambapo baadhi
ya Waislamu wameandamana kupinga kitendo cha kijana huyo na kupelekea jeshi la
polisi kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao.
Waumini hao
ambao wamejiunga kutoka maeneno mbalimbali ya Mbagala wamezingira kituo cha
Polisi cha Kizuiani ambapo mtoto amesalimishwa kutokana na sababu za kiusalama.
Waumini hao
wenye hasira wanataka kijana huyo atolewa kituoni hapo la sivyo watachoma moto
kituo hicho.
Aidha kumeshuhudia
vurugu kubwa kutoka Mbagala Kizuiani majira ya saa 7 na sasa inadaiwa wakazi
waishio maeneno ya Mbagala wametandwa na hofu kutokana na vurugu hizo.
Mkazi mmoja
kutoka maeneo ya Mbande amesema kuwa
tayari kuna baadhi ya watu wameshajeruhiwa na fujo hizo zilitokea maeneo hayo
kufuatia tukio hilo .
Msemaji wa
jeshi la polisi nchini Advela Senso amesema tukio hilo limetokea wakati watoto
wawili wakicheza ambapo mtoto mmoja alimwambia mwenzake kuwa akifanya jambo
lolote baya dhidi ya Qur’uan atabadilika na kuwa nyoka.
Baada ya
mtoto huyo kudaiwa kudhalilisha Quruan alianza kutafutwa na wazazi huku wazazi
wa mtoto husika wakimbiza katika kituo cha polisi kwa ajili ya usalama.
![]() |
Picha Mojawapo ya makanisa yanayodaiwa kuharibiwa likiungua
moto.
|
Kwa upande
wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw Said Meck Sadick amewataka wakazi wa jiji
la Dar es salaam kuwa na subira kwa wakati huu ambapo vyombo vya dola
vinaendelea kulishughulikia suala hilo.
No comments:
Post a Comment