Ikiwa nyumbani Lubumbashi TP Mazembe watoka sare ya 0-0 na Mabingwa watetezi Esperance ,Mechi ikitawaliwa kwa Kadi 9 mojawapo ikiwa Kadi Nyekundu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 07, 2012

Ikiwa nyumbani Lubumbashi TP Mazembe watoka sare ya 0-0 na Mabingwa watetezi Esperance ,Mechi ikitawaliwa kwa Kadi 9 mojawapo ikiwa Kadi Nyekundu.


Kwenye Mechi za kwanza za Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI zilizochezwa hapo jana na leo matokeo yamekua ni  ya sare kwa  karibu mechi zote mbili baada ya wenyeji timu ya Sunshine Stars kutoka 3-3 na  Al Ahly ya Misri  jana ili hali  leo huko Lubumbashi TP Mazembe  nao kutoka sare ya 0-0 na Mabingwa watetezi Esperance kwenye Mechi iliyotawala kwa Kadi huku Kadi 9 zikitembezwa mojawapo ikiwa Kadi Nyekundu.


Wachezaji wa Mazembe waliopewa Kadi za Njano ni pamoja na Kilitcho Kasusula,Mabi Mputu,Stopilla Sunzu,Ngandu Kasongo na Stopilla Sunzu Kadi Nyekundu huku Wachezaji wa Esperance waliopewa Kadi za Njano ni Derbali,Traoui,Ragued na Afful.

MARUDIANO

Jumamosi Oktoba 20   
      
22:30 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v TP Mazembe - Congo, The Democratic Republic Of The [Stade El Menzah]

Jumapili Oktoba 21    
     
20:30 Al Ahly – Egypt v Sunshine Stars – Nigeria [Cairo International Stadium]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad