![]() |
Aidha mradi huo utakuwa na faida kwa Halmashauri,
Wananchi wa Wilaya ya Ngara pamoja na Watanzania; na kwamba wameahidi
kuiwezesha Halmashauri ya Wialaya ya Ngara katika miundombinu ya
barabara, hospitali, pamoja na elimu.
“Tayari
konteina moja la kompyuta linakuja kwa ajili ya kuzigawa mashuleni; kompyuta
hizo zinatupa uhakika wa watoto wetu kujifunza somo la TEHAMA; kwa hiyo unaweza
kuona jinsi uwekezaji huo utavyokuwa na faida kubwa kwetu sisi kama
halmashauri.” Alisema Bw. Bahama.
Aidha,
amesema kwamba watu wanaozunguka mradi huo, watawezeshwa katika teknolojia ya
kuzalisha kahawa, avocado, makademia na mpunga, ili waweze kuazalisha zaidi,
huku wakiwa na soko la uhakika.
|
![]() |
Naye, Mkuu
wa Wilaya ya Ngara Lt. Col. Michael
Mntenjele, amewakaribisha wawekezaji katika Wilaya ya Ngara, huku akidai
kwamba ni matumaini yake kuwa wataendelea kuja ngara, ili kuhakikisha
kwamba mkataba huo unatekelezwa kwa mafanikio ya wananchi wa wilaya ya Ngara.
Aidha,
amefafanua kwamba wenyeji wanaozunguka mradi huo, watajifunza utaalamu mpya wa
kuzalisha mazao ya biashahara kama vile kahawa, mpunga na parachichi na
kusaidia kutoa mbegu bora za mazao hayo kwa wananchi wa wilaya ya Ngara.
|

![]() |
Baada ya Serikali
ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kusaini mkataba huo imeelezwa utekelezaji wa
miradi iliyopangwa utaanza miezi mitatu ijayo na kuanza kuajiri wananchi wenye
sifa mbalimba kitaaluma ili kuharakisha malengo uwekezaji huo.
|

No comments:
Post a Comment