Wauguzi wa
Zahanati ya Kaisho iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera, wakisaidia kubeba
maboksi yenye dawa baada ya kupelekewa na Bohari ya Dawa (MSD) wilayani humo
mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Devotha Maganga, Editha Nyaruzi na Yolanda
Joseph. |
Akizungumzia
upatikanaji wa dawa kutoka MSD alisema zinapatikana kwa wakati na kuwa pamoja
na kituo hicho kuwepo na muingiliano huo wa watu kutoka nchi jirani ya Uganda
hawana ubaguzi wa kutoa huduma kwao.
"Kituo
chetu kinatoa huduma kwa watu wote bila ya ubaguzi na hatujawahi kupungukiwa
dawa kwa vile tunapo agiza dawa tunakuwa na idadi ya pande zote mbili na
kuongeza za ziada jambo ambalo limsaidia tusiwe tunapungukiwa kwa dawa zote
muhimu" alisema Dkt.Eid.
Alisema
katika kituo hicho cha afya kwenye mwezi wa sita wagonjwa wanaotibiwa ni kati
ya 50 hadi 80 kwa siku lakini kwa hivi sasa ni wagonjwa kuanzia 20 hadi 40
ingawa hakufafanua kwanini idadi hiyo inapungua katika kipindi hicho.
Mganga Mkuu
wa wilaya hiyo, Dkt. Diocles Ngaiza alisema upatikana wa dawa katika wilaya
hiyo kutoka MSD ni mzuri ukilinganisha na miaka 2015 ambapo walikuwa wakipata
asilimia 30 lakini sasa hivi ni zaidi ya 70.
Katika ziara
hiyo wilayani Kyerwa MSD ilikabidhi dawa katika Kituo cha Afya cha Murongo na
Zahanati ya Kaisho.
|
Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Kyerwa, Dkt. Diocles Ngaiza, akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu upatikaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD), mkoani humo mwishoni mwa
wiki. Kulia ni Mfamasia wa wilaya hiyo, Dominic Malabeja.
|
Tabibu wa
kituo hicho, Denis Rugemalira (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa
(MSD), Cornelia Mwillawi baada ya kukabidhi dawa katika kituo hicho.
|
Afisa Huduma
kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Cornelia Mwillawi (kushoto), akimuonesha
fomu maalumu ya kujaza baada ya kukabidhiwa dawa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha
Afya cha Murongo, Dkt.Rashid Eid (kulia), baada ya kukabidhiwa dawa mwishoni
mwa wiki. Katikati ni Tabibu wa kituo hicho, Denis Rugemalira.
|
No comments:
Post a Comment