Pia Mhe.
Naibu Waziri Kandege aliiomba familia ya
marehemu kuwa na subira kwa wakati huu mgumu wa kupoteza mpedwa wao Sperius
Eradius na kusema kuwa msiba si wao tu bali ni msiba wa taifa zima.
Aidha,
aliishukuru Serikali ya Mkoa ilivyoshughulikia tukio hilo tangu lilipotokea
Agosti 27, 2018 hadi kuupumzisha mwili wa Mwanafuzi Marehemu Sperius Eradius
nyumbani kwa baba yake mzazi Eradius Petro.
Baba yake
mlezi Mchungaji Justus Balilemwa akitoa historia ya Mwanafunzi Marehemu Sperius
Eradius alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa Mei 2005 na mara baada ya kuzaliwa
mama yake aliaga dunia na Sperius Eradius kuchukuliwa na kupelekwa Ntoma katika
Kituo cha kulelea watoto yatima na baada ya mwaka mmoja alimchukua mtoto huyo
na kuanza kuishi na kumlea kama mtoto wake hadi mauti yalipomkuta Agosti 27,
2018 akiwa na umri wa miaka 13 Shuleni Kibeta Manispaa ya Bukoba.
“Kinachonisikitisha
leo hii ni kuwa tulimchukua Sperius Eradius akiwa mzima lakini leo tumerudisha
sanduku, haikuwa nia yetu tulitamani sana mtoto huyu atimize ndoto zake kwa
kuwa alikuwa mchangamfu sana na alimjua Mungu kwa kuimba na kumtukuza Mungu
katika Kwaya mbalimbali mfano kwaya ya Kagoma.” Alimalizia kwa uchungu mkubwa
baba mlezi wa Sperius Eradius Mchungaji Justus Balilemwa.
|
Baba yake
mzazi Marehemu Sperius Eradius, Eradius Petro akitoa neno kwa wananchi
waliofika kumfariji katika mazishi hayo alisema yeye anamwachia Mungu kwa
yaliyotokea bali anaishukuru Serikali kwa kulifuatilia tukio hilo kwa karibu
sana. Pia na kutoa ushirikiano nyumbani kwa baba mlezi tangu tukio linatokea
hadi kwenye mazishi ya Sperius Eradius.
Serikali ya
Mkoa wa Kagera tangu kutokea kwa tukio hilo la mauaji ya Mwanfunzi Sperius
Eradius (13) Agosti 27, 2018 imekuwa ikigharamia mahitaji yote katika familia
ya baba mlezi na kugharamia jeneza la kumhifadhia marehemu pamoja na usafiri wa
kusafirisha mwili wa marehemu, familia, ndugu na jamaa wa Sperius kutoka Kibeta
kwenda Mubunda Kijiji Kitoko kwa ajili ya Mazishi.
Aidha, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Kandege alitoa Shilingi Milioni mbili kwaniaba ya Serikali.
|
No comments:
Post a Comment