Baadhi ya
mafuvu ya wanayamapori katika Pori la Akiba la Burigi katika eneo la Nyungwe. |
Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la
Burigi na eneo la Wananchi katika eneo la Nyungwe na Ofisa Mwenye wadhifa wa
Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na Hifadhi
za Taifa Tanzania kusimamia Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa
Hifadhi za Taifa, Damian Saru ( wa kwanza kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.
|
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde. |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana kwenye mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo. |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bihalamulo pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo. |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) akioneshwa eneo la Ziwa Burigi katika eneo la Nkonje na Meneja wa Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo. |
Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga
akisaini kitabu cha wageni i katika eneo la Nyungwe wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana mapori hayo katika ziara
yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU
HELELA-WMU)
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA.
Bodi ya
Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu
matumizi ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike
kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa
miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi
za Taifa.
Hatua hiyo
imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha hadhi Mapori ya
Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za
Taifa kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla
wakati alipokuwa akihitimisha bajeti ya Wizara mwezi Mei
mwaka huu Bungeni mjini Dodoma.
Ofisa Mwenye
Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana mbele ya Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga wakati
alipotembelea mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa
ni ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili
ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori
hayo.
Alitaja
fedha hizo kuwa zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga
miundo mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa
kupandisha hadhi mapori
Damian Saru,
Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha
taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji
zilizofikiwa katika mapori hayo.
Alimweleza
kuwa askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza
nguvu.
Mashine ya
kutengeneza barabara ' Motor Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza
barabara.
Pia,
Alimweleza Naibu Waziri huyo ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari
manne, mahema silaha, GPS vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha
utendaji kazi
Kufuatia
utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio
yaliyopatikana katika kIpindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika
kipindi cha wiki mbili pamoja na ng'ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Pia ,
Alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa ujangili wamekatwa.
Aidha, Saru
alitaja aina za vifaa vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili
pamoja na baiskeli zopatazo 10.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri , Mhe.Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA kwa
ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kwa nzuri
waliyoifanya.
|
No comments:
Post a Comment