Mhandisi TARURA Awataka Wananchi Ngara kutunza Barabara zilizofanyiwa Matengenezo Milioni 592 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 15, 2018

Mhandisi TARURA Awataka Wananchi Ngara kutunza Barabara zilizofanyiwa Matengenezo Milioni 592 .

Zaidi ya Shilingi Milioni 592.519 zimetumika katika mategenezo ya barabara 32 zenye urefu wa kilomita  86, na ujenzi wa makaravati 20 katika barabara 14 katika kipindi cha mwezi Julai 2017/2018.

Mhandisi wa TARURA kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Christopher Masunzu amebainisha hayo  hivi karibuni na kwamba Matengenezo hayo yamegawanyika katika makundi matano.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni Matengenezo ya kawaida (routine maintenance) yaliyogaharimu jumla ya Shilingi Milioni 66.8  katika barabara zilizoko kata za Kanazi, Mugoma, Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Rulenge, Kibogora, Keza, Murukurazo na Mabawe.

Matengenezo ya sehemu korofi (Spot improvement) katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Mbuba, Kibimba na Nyamiaga zilizogharimu shilingi milioni 30.5
Matengezo ya muda maalumu (periodic maintenance) yametumia shilingi milioni 150, katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Bukiriro, Murusagamba, pamoja na Ntobeye.

Bw.Christopher Masunzu  amesema matengezo mengine yalikuwa ya barabara 3 za lami zenye urefu wa kilomita moja zilizojengwa katika Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara na kutumika jumla ya shilingi za kitanzania Milioni 304,297,239.00.

Katika mwaka huo wa fedha 2017/2018  TARURA wilaya ya Ngara walifanikiwa kujenga makaravati (Culverts) yapatayo 20 katika barabara 14 katika kata za Mamlaka ya Mji Mdogo Ngara, Nyamiaga, Kabanga, Kasulo, Bukiriro Murukulazo, Kibimba, Mugoma pamoja na Ntobeye.

Aidha, Mhandisi huyo wa TARURA amesema Makaravati hayo yamegharimu jumla ya shilingi Milioni 40,875,200/=; huku akitoa wito kwa wananchi kuzitunza barabara hizo kwani zimetumika fedha nyingi ambayo ingeweza kufanya kazi nyingine za maendeleo.

Amewaonya wananchi wenye tabia ya kulima kwenye hifadhi ya barabara kuacha tabia hiyo mara moja, kwani wanasababisha kuziba kwa mitaro kunakopelekea kuharibika kwa miundombinu hiyo kwa  muda mfupi hasa wakati wa mvua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad