
Wananchi
Mkoani Kigoma wamelitaka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani
kuchukua hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani Madereva na watu wote
wasio zingatia sheria za usalama barabarani.
Kauli hiyo
imekuja kufuatia ajali katika eneo la Gungu Manispaa ya Kigoma ujiji kutokana
na uzembe wa dereva wa basi hilo ambae hakuchukua tahadhari wakati akivuka eneo
la reli.
Katika hatua
nyingine Wananchi hao wamesema uwepo wa baadhi ya Askari Polisi wa usalama
barabarani wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakitimiza majukumu yao
wamekua chanzo kikubwa cha ajali.

Kwa upande
wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma ASP Martin Otieno amesema Jeshi hilo halitawavumilia baadhi ya Madereva wanaokiuka sheria za
usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi juu ya tuhuma za baadhi
ya Askari Polisi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.
June 6,2018 ilitokea ajali na Watu 10 kufariki dunia
na wengine 35 kujeruhiwa kufuatia Basi namba T 885 DLD la Prince Hamida
lililokuwa likitoka Kigoma kuelekea Tabora kugonga na treni ya mizigo mkoani
Kigoma katika eneo la makutano ya barabara na reli eneo la Gungu katika
Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Basi hilo la Prince Hamida hufanya safari zake
kati ya Mikoa ya Kigoma na Tabora.
No comments:
Post a Comment