![]() |
Kaimu
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kumuzuza Bw Marthon Christopher akionesha moto ulivyounguza Nyumba ya Mzee
Petro huku baadhi ya Wananchi wakishuhudia.
|
![]() |
Nyumba
saba zimeungua kwa nyakati tofauti katika kijiji cha Kumuzuza wilayani Ngara
mkoani Kagera huku kukitokea vifo vya watoto wawili ndani ya familia moja
katika Mazingira ya kutatanisha vikihusishwa kwa imani za kishirikina.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kumuzuza Bw
Marthon Christopher amesema Mtoto wa kwanza amefariki mwezi mmoja uliopita
na mwingine amefariki juzi na wote ni wajukuu wa mzee mmoja aitwaye Petro Sabimihana mwenye umri wa miaka
68.
Bw Christopher amesema watoto
waliofariki mmoja ana umri wa miaka minane mwingine miaka miwili na kukutwa
chumbani ndani ya nyumba ya mzee huyo ikiwa imefungwa na kwamba nyumba saba
zimeungua kuanzia Novemba mwaka jana (2017) na iliyoungua jana chanzo chake
hakijafahamika.
|

![]() |
Kwa upande
wake Mzee Petro Sabimihana alikiri
kuijiwa na miujiza na kuunguliwa na vitu mbalimbali ndani ya nyumba yake na
kwamba hadi sasa hana nguo, chakula wala vyombo na moto huo huunguza majiko,
vyoo bila kujua chanzo chake.
Alisema alijitahidi kufanya maombi akisaidiwa
na Padri Pamphilius Kitondo
ikashindikana ambapo miujiza hiyo hupoteza wajukuu wake kupitia chumba
anacholala hata kama kimefungwa hukuta wamefariki.
|

![]() |
Baadhi ya
Wananchi wa kijiji hicho wamekumbwa na taharuki kuhofia usalama wa maisha yao
kwa matukio hayo ya vifo na nyumba kuungua wakiomba vyombo vya usalama kufika
kuimarisha amani na utulivu.
|
![]() |
Jeshi la Polisi wilayani Ngara limethibitisha
kutokea kwa matukio hayo ambapo mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amewataka Wananchi
kuishi kwa amani na utulivu na kwamba serikali haiamini kuwepo vitendo vya
ushirikina.
Na -Shaaban
Ndyamukama-Ngara.
|
No comments:
Post a Comment