Kaimu Mkuu wa Mkoa Mhe Kinawli Akimkabidhi Pasipoti ya Kielekitroniki Baba Askofu Lwoma wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Bukoba. |
Katibu Tawala Mkoa Kagera CP Diwani Athuman Akisubiri Kuchukuliwa Alama za Vidole Kukamilisha Hatua za Pasipoti ya Kielekitroniki. |
Mkuu wa Mkoa
Kagera Mhe. Kijuu na Katibu Tawala Mkoa CP Diwani Athuman Wakishiriki Hatua za
Kupata Pasipoti ya Kielekitroniki.
Awali Kamishina wa Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga alisema kuwa mara baada
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli kuzindua Pasipoti za Kielekitroniki Januari 31, 2018
Pasipoti hizo zilikuwa zinatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam na
Zanzibar tu lakini sasa mikoa imeanza
kuzindua na kutoa Pasipoti za Kielekitroniki.
Kamishna Kihinga alisema kuwa tayari Pasipoti za
Kielekitroniki zimeanza kutolewa katika mikoa ya Dadoma, Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na sasa Mkoa wa Kagera ambao uzinduzi umefanyika leo
Juni 8, 2018.
|
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoriki la Bukoba Desiderius Lwoma na Askofu Msaidizi Kilaini Wakifurahia Pasipoti zao za Kielekitriniki Baada ya Kuzinduliwa Rasmina Kukubidhiwa. |
Askofu
Msaidizi wa Jimbo Katoriki la Bukoba Akitoa Neno la Shukrani Baada ya Uzinduzi
na Kukabidhiwa Rasmi Pasipoti za Kielekitroniki Mkoani Kagera.
Kwaniaba ya
Viongozi na wote waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika uzinduzi Mkoani
Kagera Baba Askofu Methodius Kilaini ,Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoriki la
Bukoba aliishukuru Serikali na Idara ya Uhamiaji kwa kutoa Pasipoti za
Kielekitroniki kwa wananchi na alisema kuwa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera
imejipanga vizuri hasa katika mapokezi ya wananchi na huduma.
“Tunashukuru
sana na nimeikagua Pasipoti yangu ya Kielekitroniki na kugundua kuwa ni
pasipoti nzuri sana tena sana, sasa itatusaidia sisi kama Viongozi wa
dini na wananchi katika kusafiri, naiona Tanzania ikiendana na mataifa mengine
katika masuala ya mitandao.” Alisistiza Baba Askofu Kilaini.
|
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Deodatus Kinawilo Akisoma Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti ya Kielekitriniki Mkoani Kagera Kwaniba ya Mkuu wa Mkoa. |
Maofisa wa
Idara ya Uhamiaji Wakisikiliza Kwa Umakini Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti za
Kielekitroniki Mkoani Kagera.
Naye Afisa
Uhamiaji wa Mkoa wa Kagera Abdalah Towo akiongea na mhadhara wa wananchi
waliohudhuria uzinduzi wa Pasipoti za Kielekitroniki aliwakumbusha Maafisa
wenzake katika Wilaya kuwa Elimu imetolewa ya kutosha kwao na ni lazima kuwaelimisha
wananchi na kuwaongoza katika kupata Pasipoti za Kielekitroniki katika Wilaya
zao.
Pia
Bw. Towo alitoa rai kwa wananchi waliopatiwa Pasipoti za Kielekitroniki katika
uzinduzi huo kuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wenzao na kuhakikisha
wanapitia michakato yote wao waliyoipitia na kama kutatokea mwananchi anasema
yeye hajapitia mchakato huo na amepata Pasipoti ya kielekitroniki aripotiwe
mara moja katika Ofisi za Uhamiaji ili hatua zichuliwe mara moja.
Aidha, Bw.
Towo alisema katika uzinduzi huo zilitolewa Pasipoti za Kielekitroniki 101 kwa
Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, Wazee, Watumishi na Wananchi.
|
Picha ya Pamoja .
Unahitaji
nini ili Upate Pasipoti ya Kielekitroniki?
Gharama ya
Pasipoti ya Kielekitroniki ni Shilingi 150,000/=, Utajaza fomu hata ukiwa
nyumbani ambayo inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz .
Viamabatanisho ni pamoja na Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa cha
kwako na cha mzazi wako mmoja, Barua ya utambulisho kutoka kazini
kwako/Mtendaji wa kata, Kitambulisho cha Kazi/mpiga kura, na picha tatu
pasipoti size.
|
No comments:
Post a Comment