![]() |
Wananchi wa
kijiji cha Kyenda kata ya Murukulazo wilayani Ngara mkoani Kagera wameiomba
serikali kuchukua hatua juu ya maji yaliyojaa mto ruvubu na kufurika kwenye
mashamba yao.
Wakizungumza
na Radio Kwizera Kijijini hapo wamesema hali ya mavuno kwa msimu huu ni ngumu
kwao baada ya maji kufurika kwenye mto huo na mto Kagera baada ya kuzibwa na
mradi wa umeme Rusumo NELSAP.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw Ferdinand Festo Masenge amesema mpaka
sasa zaidi ya Wananchi 300 wamekwisha athirika na maji hayo ambayo yameharibu
kiasi kikubwa cha mazao mashambani.
Naye Diwani
wa Kata ya Murukulazo ( CCM ) Bw Mukiza Byamungu amesema mbali na athari
za Kilimo lakini pia Sekta ya Afya, Elimu na Biashara zimeharibiwa kwa kiasi
kikubwa kwakuwa baadhi ya walimu, wauuguzi na wanafunzi hutegemea kivuko ambacho
kwasasa hakina uwezo wa kutoa huduma.
|
Post Top Ad
Saturday, June 09, 2018

Wananchi 300 waathirika na Kujaa Maji ya Mto ruvubu Wilayani Ngara,Kagera.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
Viongozi Kagera - ''Marufuku Kutoa Hati za Kusafiria za Kielektroniki Kinyume na Sheria''.
Makala Iliyopita
Magazetini June 9,2018 Utasoma Vijuso vya Siasa,Kijamii, Uchumi ,Michezo na Burudani.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment