Kamishna wa
Uraia na Pasipoti Gerald Kihinga (Kushoto) Akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe. Kinawilo Pasipoti ya Kielekitroniki
Baada ya Uzinduzi Jana June 8,2018.
Serikali ya
Tanzania imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria Watumishi wa Uhamiaji
watakaobainika kushirikiana na viongozi na watendaji wa vijiji kutoa hati za
kusafiria za kielektroniki.
Hayo
yameelezwa na Kamishina wa Uhamiaji anayeshughulikia Hati na Uraia Bw Gerard Kihinga wakati wa uzinduzi wa
huduma ya Paspoti ya kielektroniki Mkoani Kagera June 8,2018 uzinduzi
uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Bukoba.
Amesema hati
hiyo ni kwa ajili ya Watanzania pekee lakini wapo raia wa kigeni wangependa
kutumia pasipoti hiyo kuishi nchini kinyume cha sheria ambapo amewataka
watumishi kuwa waaminifu.
|
Maofisa wa
Idara ya Uhamiaji Wakisikiliza Kwa Umakini Hotuba ya Uzinduzi wa Pasipoti za
Kielekitroniki Mkoani Kagera. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amewataka Maafisa Uhamiaji kufanya kazi kwa Uaminifu na Uadilifu huku akiwataka Wananchi kujitokeza kujiandikisha ili kupata hati hiyo. |
Picha ya
Pamoja .
Unahitaji nini ili Upate Pasipoti ya
Kielekitroniki?
Gharama ya
Pasipoti ya Kielekitroniki ni Shilingi 150,000/=, Utajaza fomu hata ukiwa
nyumbani ambayo inapatikana katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji
www.immigration.go.tz .
Viamabatanisho
ni Pamoja na Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa cha kwako na cha mzazi
wako mmoja, Barua ya utambulisho kutoka kazini kwako/Mtendaji wa kata,
Kitambulisho cha Kazi/Mpiga Kura, na Picha tatu Pasipoti size.
|
No comments:
Post a Comment