Mkuu wa
wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti akionesha hatimiliki kwa Wananchi
kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Picha zote Rhoda Ezekiel.
Halmahsuri
ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma imeanza zoezi la ugawaji wa hati miliki za
kimila katika vijiji vya Mugera, Kajana na Katundu katika kata ya Mugera na
Kajana katika kaya 1025 hati ambazo zitasaidia kupunguza migogoro ya ardhi
katika wilaya na mkoa kwa ujumla.
Akikabidhi
hati miliki hizo kwa kaya 50 za mfano June 3, 2018 katika kijiji cha Muhegera
kata ya Mugera wilayani humo, zinazotolewa na mradi wa usimamizi wa maliasili
kwa ajili ya kuongeza kipato kwa Mwananchi unaotekelezwa na Serikali ya
Tanzania na Ubelgiji chini ya shirika la ENABEL, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Kigoma, Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema katika
kesi 10 zinazofika ofisini kwake kati ya hizo 8 ni za migogoro ya ardhi na
mbili ni za urithi.
Gaguti alisema mradi huo utasaidia usalama wa wananchi na kupunguza
migogoro ya ardhi ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na
wengine kubaki wakiwa walemavu kwa kugombania ardhi.
Brigedia
Jenerali Marco Gaguti amewataka Viongozi
wa vijiji kusimamia ipasavyo maeneo ya huduma za kijamii yaliyopimwa kwa ajili
ya shughuli za ufugaji na kilimo yatumike kwa lengo lililokusudia na wananchi
waelekezwe namna bora ya kuyatumia na kuepusha migogoro kwa wananchi. |
No comments:
Post a Comment