
Mbunge wa Jimbo
la Ngara mkoani Kagera Mhe.Alex
R.Gashaza akikagua ujenzi wa Vyumba vya Madarasa,Mabweni na Matundu ya Vyoo
katika Shule ya Sekondari Murusagamba.
Picha Na –Maktaba
Yetu.

Mbunge wa
jimbo la Ngara mkoani Kagera Mhe.Alex
Gashaza ametoa shilingi milioni 2 za mfuko wa jimbo hilo kukiwezesha
Kikundi cha walemavu kata ya Rulenge
wilayani humo kuendeleza miradi yao.
Katibu wa Mbunge
wa Jimbo la Ngara anayesimamia tarafa ya Rulenge na Murusagamba Bw Lengo Kapfusi amesema kikundi hicho
kinajihusisha na Ufugaji wa Mbuzi na upandaji wa Miti pamoja na kilimo cha
Bustani.
Bw Kapfusi amesema mfuko huo pia umetoa shilingi
milioni 4 kuunga mkono Juhudi za Wananchi wanaojenga vyumba vya Madarasa katika
shule ya msingi Rulenge na Mubwilinde baada ya wanajamii wa maeneo hayo
kuchangia nguvu zao.
Amewataka walengwa
waliopatiwa fedha hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kupata Tija
katika Maendeleo endelevu.
Aidha
Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu Rulenge Bw
Charles Kagambokabi amekiri kupokea fedha hizo na kwamba zimetumika kununua
mbuzi 11 na fedha nyingine zimeelekezwa kwenye shughuli za ujasiriamali na
kukopeshana.
No comments:
Post a Comment