Taswira Namna Yanga SC ikiondoshwa na Kakamega Boys -SportPesa Super Cup 2018 nchini Kenya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 03, 2018

Taswira Namna Yanga SC ikiondoshwa na Kakamega Boys -SportPesa Super Cup 2018 nchini Kenya.

Kikosi cha Yanga SC kimeondoshwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Kakamega HomeBoys, mchezo uliopigwa leo June 3, 2018 mjini Nakuru, Kenya.

Kakamega wamejipatia mabao yao kupitia kwa Allan Wanga aliyefunga mawili huku moja likiwekwa kimiani na Opondo. 

Bao pekee la Yanga SC limewekwa kiminiani na Matheo Anthony kwa njia ya mpira wa faulo.
Matokeo hayo yanaibakiza Kakamega huku Yanga SC ikiyaaga rasmi mashindano na jumla ya timu 3 sasa kutoka Tanzania ambazo ni JKU, Singida United na Simba SC zikisalia.

Muda mchache kuanzia sasa JKU kutoka Zanzibar itakuwa inakipiga na na mabingwa wa Ligi Kuu Kenya msimu uliomalizika, GorMahia FC.
Simba SC watashuka dimbani kesho Jumatatu June 3, 2018 kucheza dhidi ya Kariobang Sharks, mchezo ukianza majira ya saa 9 alasiri.

Wakati huo wachezaji Shiza Kichuya na Mohamed Rashid wameondoka pamoja leo June 3,2018 kuelekea Nakuru ili kujiunga na kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad