![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea
Ndagala akipokea Maelezo ya Mazao ya mboga mboga yanayo limwa na wakimbizi
Kambi ya Nyarugusu katika mradi wa utunzaji wa Mazingira.
Amesema katika kupambana na hali hiyo Shirika
la uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa mazingira kambini ( CEMDO)
Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR
wameandaa utaratibu wa upandaji wa miti 1,425,223 katika Vijiji 13
vinavyozunguka Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa mwaka 2017/2018 , kugawa
majiko banifu kwa kaya 9600 za wakimbizi.
Pamoja na majaribio ya ugawaji wa gesi kwa kaya 3180 lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni yanayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na kuboresha mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa uoto wa asili unaotokana na ukataji miti ovyo. |
![]() |
Mmoja wa Wakimbizi akimuelezea Mkuu wa Wilaya
namna wanavyo yatumia Majiko Banifu kuhakikisha hawaharibu Mazingira.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa
Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema kauli mbiu ya
maadhimisho ya mazingira ni "MKAA NI GHARAMA;
TUMIA NISHATI MBADALA",Ambapo amesema kauli hiyo inasaidia
utunzaji wa misitu na mazingira, lakini kumekuwa na tabia ya baadhi ya
wakimbizi kupewa majiko banifu na gesi kwenda kuuza kwa Watanzania
ilikujipatia fedha na kuendelea kuharibu mazingira na kuwataka wakimbizi kuacha
tabia hiyo na kuendelea kutumia majiko yaliyotolewa na shirika hilo.
Naye Rais wa Wakimbizi Kambi ya
Nyarugusu Abilola Angelique amesema wao kama wakimbizi hawana budi
kuunga mkono jitihada zinazofanywa na mashirika yanayo wahudumia, kwa kuwa
wanapotunza mazingira hata wao wanaendelea kunufaika kwani watatumia ardhi hiyo
kulima mazao ya mboga mboga kwa ajili ya kujikimu na watoto wao.
Amewaomba wakimbizi wenzake kuendelea kusimamia utunzaji wa mazingira. |
No comments:
Post a Comment