Simba SC na Gor Mahia Fainali ya SportPesa Super Cup 2018 -June 10, 2018 Uwanja wa Afraha, Nakuru. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 08, 2018

Simba SC na Gor Mahia Fainali ya SportPesa Super Cup 2018 -June 10, 2018 Uwanja wa Afraha, Nakuru.

Mashabiki wa Gor Mahia.

Mabingwa  watetezi, Gor Mahia ya Kenya rasmi sasa watakutana na Simba SC ya Tanzania katika fainali kali ya SportPesa Super Cup 2018  Jumapili ya June 10, 2018 kwenye Uwanja wa Afraha, Nakuru.
Gor Mahia wanaenda fainali hiyo baada ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Singida United katika mchezo nusu fainali ya pili leo June 7, 2018 Uwanja wa Afraha,kwa  mabao ya Meddie Kagere.

Simba SC  nao wameenda fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Kakamega Homeboyz baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Waliofunga penati za Simba SC leo ni viungo, Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomary Kapmbe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude, wakati Gor Mahia walipiga juu penati yao ya mwisho.
Kikosi cha Simba SC.

Katika mashindano hayo Simba SC ilipenya kwa penati 3-2 baada ya sare ya 0-0 pia dhidi ya Kariobangi Sharks kabla ya kuendeleza ushindi wa staili hiyo mbele ya Kakamega iliyowatoa Yanga SC  ya Tanzania pia kwa kuwachapa 3-1.   
 
Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Jumapili na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 

Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500. 

Bingwa mtetezi ni Gor Mahia ambayo mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad