Licha ya Serikali kupiga marufuku Utumiaji
wa Mifuko ya Plastiki ,bado mifuko hiyo inatumiwa na Wafanyabiashara Sokoni.
Serikali
Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga inatarajia kutumia Jeshi la akiba la Mgambo
kukabiliana na Watu wanaotupa hovyo Mifuko ya Plastiki kama njia ya
kutekeleza Sheria ya Mamlaka ya hifadhi ya Mazingira ya mwaka 2017.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Bw
Fadhil Nkurlu wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake na
kwamba wale watakaokamatwa wakitupa taka
hovyo watafikishwa mahakamani.
Amesema
mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira NEMC wametoa waraka wao wa kuzuia matumizi
ya mifuko ya prastiki lakini watu wanaendelea kutumia mifuko hiyo kinyume
cha sheria. 
Mrundikano wa Taka za Mifuko ya Plastiki
–Picha Na Maktaba yetu.
Nao Baadhi
ya Wakazi wa mji wa Kahama wameitaka halmashauri ya mji wa Kahama kuweka vitu
vya kutunzia taka mitaani ambapo wamesema vifaa walivyopewa na kampuni ya
uchimbaji madini ya ACACIA Buzwagi wamevitelekeza ofisini badala ya kuvisambaza
kwenye mitaa ya mji huo ili vitumike
kutunzia taka.
Na–Radio Kwizera.
|
No comments:
Post a Comment