![]() | |
Kamati ya
Siasa ya Mkoa wa Kagera ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Bi.
Constancia Buhiye imetembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Mwaka 2015.
|
![]() |
Gharama za
Mradi waliowekeza ni Shilingi milioni 40 ambapo Halmashauri ya wilaya ya Muleba
iliwakopesha kiasi cha Shilingi milioni 21.
Mradi una
Jumla ya Vijana 17 ambao wote ni wa Kiume.
Soko lao wanauzia Wananchi na wanasafirisha Mtukula wilayani
Misenyi ambalo ndilo Soko lao kuu. Mipango ya baadaye ni kuwa na kiwanda cha
kukamua Juisi.
|

No comments:
Post a Comment