Kilimo Cha Maharage -Ngara. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, June 11, 2018

demo-image

Kilimo Cha Maharage -Ngara.

.com/simgad/
35148070_1890567964316438_2792643355685683200_n
Na Shaaban Ndyamukama –Ngara.

Wakulima wa zao la maharage wameshauriwa kulima na kupanda mbegu ya aina moja shambani kwa lengo la kupata mavuno bora yanayoweza kuwaingizia kipato kwa biashara badala ya kutegemea matumizi ya chakula pekee ndani ya familia.

Ushauri huo umetolewa na diwani wa kata ya Rulenge wilayani Ngara Hamisi Baliyanga  wakati akizungumza na waandishi wa habari za kilimo huku akihamasisha  wakulima wanaojiandaa kulima  maharage ya rangi mchanganyiko katika  msimu wa kilimo cha mabondeni.

Bw Baliyanga amesema maharage ya rangi mchanganyiko yanawapunja wakulima kibiashara ukilinganisha na  wanaovuna rangi moja wakati hatua za utayarishaji wa shamba hadi kuvuna unafanana kati ya mkulima mmoja na mwingine.

Katika msimu wa mavuno rangi moja inauzwa Shilingi 1200 hadi shilingi 1500 tofauti na rangi mchanganyiko yanayouzwa Shilingi 500 mpaka shilingi 600 wakati maandalizi na hatua za kilimo zinafanana” Amesema Baliyanga
 35051867_1890567867649781_7092642905952616448_n
 35071213_1890567980983103_80271843545579520_n
Pia Afisa ushauri wa kilimo kata ya Rulenge wilaya ya Ngara  Bw Esau Nyamuziga amewataka wakulima wa maharage  kuvuna zao hilo mashambani kuepuka upotevu wa mavuno  na kupata hasara katika mapato na matumizi ya  mbegu.

Nyamuziga amesema wakulima hawana budi kutambua gharama za  kilimo katika msimu mwingine   na kwamba uvunaji wa maharage  kutoka shambani na kuyaandalia nyumbani   wanapata hasara ya kubaki  baadhi ya mabegu shambani.

Aidha ameshauri uvunaji huo ufanyike mapema kabla ya kukauka kwa muda mrefu kwani maharage hupasukia kwenye maganda na mengine hupotea wakati wa usafirishaji kwa kutumia kichwa, baiskeli na vyombo vingine vya usafiri.

“Uvunaji mwingine wa maharage ni kujihadhari na upuraji kwa kutumia fimbo nzito katika sehemu ngumu kwani yanaweka kupasuka punje zake kwa kutumia nguvu na kusababisha kukosa soko kibiashara” Amesema Nyamuziga.
 35123940_1890568427649725_8841529090390360064_n
 35162252_1890568474316387_315865059022602240_n
Wakizungumza na Radio kwizera  baadhi ya  wakulima  wamesema sababu ya  kupanda mbegu mchanganyiko ni kutokana na ardhi wanayotumia kutokuwa na rutuba hivyo kutegemea mavuno  ya kubahatisha  katika misimu mbalimbali.

Mmoja wa wakulima hao ni Mzee Nicolaus Kanuma ambaye amesema baadhi mbegu zinastahimili mvua na nyingine ukame hivyo wanapochanganya wanapata mavuno kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Afisa kilimo wilayani Ngara Bw Costantine Mudende amesema wakulima wilayani Ngara wataepuka kulima mbegu mchanganyiko za maharage watakapoanza kupata mbengu mpya za aina tano ambazo zimeanza kufanyiwa majaribio.

 Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni kanali Michael Mntenjele ameshauri wakulima kutumia Radio Kwizera kupata elimu ya kilimo  na kwamba radio hiyo izingatie ratiba ya wakulima  itakayonufaisha walengwa wa kipindi husika.
 35205577_1890568507649717_709139739550154752_n

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *