![]() |
Choo cha
Kisaa cha Wanafunzi Katika Shule ya Msingi Mtamaa Manispaa Ya Singida mkoani Singida.
Picha na Maktaba yetu.
|
![]() |
Choo cha
Wasichana.
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job
Ndugai amesema watahakikisha wanajenga vyoo vya mfano katika kila
halmashauri kote nchini kwa wanafunzi wasichana na watu wenye mahitaji maalumu
ili waepukane na changamoto zinazowakabili.
Spika Ndugai amesema hayo bungeni Dodoma
alipozungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kwa sasa wataanza kukusanya
fedha za ujenzi huo kupitia zoezi la kuosha magari .
Kwa mujibu
wa Spika Ndugai zoezi hilo
litahusisha wabunge wote pamoja na mawaziri ili kufikia lengo lililokusudiwa.
|
![]() |
Choo bora katika Shule ya Msingi Unyankindi
Manispaa ya Singida kilichojengwa na shirika la SEMA la mkoa wa Singida.
Katika hatua
nyingine, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi mbalimbali Nchini wamekutana na
kufanya kongamano lenye lengo la kuweza kuboresha taaluma zao wakiwa kama
Walezi wa Watoto Wanafunzi wawapo Shuleni sambamba na kujadiliana na mabadiliko
ya ufundishaji kwa njia ya kisasa zaidi.
Kongamano
hilo limefanyika jijini Dar es Salaama ambapo limekutanisha Walimu Wakuu wa
Shule za Msingi zaidi ya 200 wengi wakiwa Wakuu wa Shule za Msingi binafsi
ambapo wampatiwa mada zenye kujenga taalum yao kulingana na wanafunzi
wanaowafundisha.
|
No comments:
Post a Comment