Wakizungumza na Radio Kwizera
sokoni hapo, baadhi ya wafanyabiashara Bi Lidia Deus na Devota Afready wamesema
kutokana na harufu mbaya inayotokana na choo hicho imeathiri biashara zao za
migahawa kutokana na wateja wao kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko.
|
Pia
wameiomba Serikali kuwarekebishia miundombinu ya choo hicho ili kuepuka
magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kujitokeza na kusababisha kufungiwa kwa
biashara zao.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bw. Modest Aprinali amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa
kupunguza uchafu katika soko hilo na kwamba jitihada za haraka zinafanyika
katika kuchimba shimo jingine kutokana na shimo hilo kujengwa kwenye mkondo wa
maji hali inayosababisha kujaaa kwa haraka pale mvua inaponyesha.
|
No comments:
Post a Comment