![]() |
Kituo cha Afya Kimeya ni miongoni mwa vituo 139 vya awamu ya pili ambavyo kila kimoja kilipewa kiasi cha Tsh. 400,000,000 kutoka Serikali Kuu kwa ufadhili wa World Bank kwa ajili ya upanuzi wa vituo hivyo na hadi sasa Chumba cha Upasuaji, Wodi ya Akina Mama, Nyumba ya Mtumishi, Maabara na Chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) vipo katika hatua ya umaliziaji. |

![]() |
Nyumba ya Mtumishi inayojengwa katika kituo wa Kituo cha Afya Kimeya wilayani Muleba mkoani Kagera. |




![]() |
Jengo la Kuhifadhia Maiti.
Aidha, ujenzi huu umetekelezwa na mafundi wanaopatikana katika maeneo ya
wananchi (Local) na kila jengo linafundi anayejitegemea ili kusaidia
kukamilisha ujenzi kwa muda uliotolewa.
Ujenzi huu unasimamiwa na Kamati
ya Ujenzi iliyotokana na Bodi ya Kituo cha Afya kwa kushirikiana na wataalamu
kutoka ofisi ya Mkurugenzi ambao ni Mhandisi wa Ujenzi, Afisa Manunuzi, Mganga
Mkuu na Afisa Mipango.
|
![]() |
Ujenzi wa Wodi ya Akina Mama katika
Kituo cha Afya Kimeya
|
![]() |
Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Kimeya na ujenzi huo unaotakiwa kukamilika
ifikapo tarehe 31/05/2018.
|
No comments:
Post a Comment