Shabiki wa
Liverpool Pichani Juu na Chini akisikitika kwa machungu baada ya kushuhudia uwanjani May 26, 2018
kilichowapata Liverpool kwa kukubali kipigo cha mabao 3 kwa 1kutoka kwa Real
Madrid.
|
Mchezo huo
wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017/2018 uliipa Real Madridi
Ubingwa huo dakika ya 51 kwa uzembe wa mlinda lango wa Liverpool Loris Karius ulimfanya Karim Benzema kuwapa Madrid bao la
uongozi, bao hilo ni la 56 kwa Benzema
na anakuwa mchezaji wa pili wa Kifaransa kufunga katika fainali ya Klabu Bingwa
Ulaya baada ya Zinedine Zidane.
|
Dakika ya 55
Sadio Mane aliisawazishia Liverpool
na hili likiwa bao lake la 10 katika Mashindano haya ya Klabu Bingwa Ulaya
msimu huu na la 20 kwa msimu huu, ambapo dakika ya 61,Kocha Zinedine
Zidane alimnyanyua Gareth Bale
aliyekuwa benchi na Gareth Bale
alifunga mabao mawili, na mabao ya Bale yanamfanya
kuwa mchezaji wa kwanza kuingia kama sub na kufunga mara mbili na
kuufanya mchezo kumalizika kwa Real Madrid kuibuka kidedea kwa mabao 3-1 huku Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza
kubeba Ubingwa wa Ulaya mara tatu mfululizo.
|
Real Madrid wanakuwa timu ya kwanza kubeba kombe
la Klabu Bingwa Ulaya mara 3 mfululizo
baada ya Bayern Munich 1974-1976, na
timu za Uingereza sasa zinakuwa zimepoteza katika fainali 7 za mwisho za Ulaya
dhidi ya timu kutoka Hispania.
|
No comments:
Post a Comment