
Idara ya
afya wilayani Ngara Mkoani Kagera inakabiliwa na upungufu wa Wauguzi na Waganga
Wafawidhi katika Zahanati, Vituo vya Afya
na Hospitali kwa ajili ya kutoa huduma bora za matibabu kupunguza
changamoto za vifo vinavyojitokeza ndani ya Jamii wilayani humo.
Taarifa hiyo
imetolewa na mmoja wa Wauguzi ,Bw.
Richard Alphonce wakati akisoma risala ya siku ya wauguzi iliyoadhimishwa
Jana May 30, 2018 badala ya May 12,
mwaka huu kutokana na sababu zisizozuilika .
Bw. Alphonce amesema pamoja na utoaji huduma, Wauguzi
wanaohitajika wilayani Ngara ni 388 kati ya hao waliopo ni 242 na upungufu
uliopo ni Wauguzi 146 na kwamba upungufu huo unachangia Wananchi kuchelewa
kupata huduma za afya.

Pichani wauguzi wakiwa katika Maandamano ya pamoja
kuadhimisha siku ya Wauguzi.

Aidha Muuguzi
mkuu wa wilaya hiyo Triphonia Rusilibana
aliwataka Wauguzi Vijana kuwa na kauli nzuri kwa Wagonjwa kwa kutanguliza upendo, kufanya
kazi wakizingatia misingi ya kitaaluma ambazo ni taratibu, kanuni na sheria za
kazi.
Pia
aliwataka kutanguliza uvumilivu katika kutekeleza na kutimiza wajibu wa kiutendaji
lakini watumie nafasi zao kujiendeleza kitaaluma badala ya kuridhika na elimu
ya ngazi ya cheti ili waweze kupata daraja kubwa kulitumikia taifa.

Pichani wakwanza kutoka kushoto ni Mganga Mfawidhi
wa Hospitali ya Murgwanza Dr.Remmy wapili ni Dr.David Mapunda na watatu ni
Muuguzi mkuu wa wilaya ya Ngara Bi.Triphonia Rusilibana.

Hata hivyo
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo ya Ngara mkoani
Kagera ambaye ni Mratibu wa Afya ya Kinywa na Meno Dkt. David Mapunda amewasihi kufanya kazi kwa nidhamu , upendo na
huruma ili husaidia kufariji mgonjwa hata kama mwili wake unakaliwa na maumivu
hivyo kumuongezea matumaini na siku za kuishi bila kukata tamaa au kulazimika
kutumia dawa zisizo na vipimo.

Wauguzi wakila kiapo kujikumbusha maneno ya
utumishi bora katika utendaji kazi hasa wakimuenzi mwanzilishi wao Frolence
Night Ngare.
Picha/Habari Na Radio Kwizera Ngara.





No comments:
Post a Comment