NESCH MINTEC -Wachimbaji Tumieni Maabara za Kisasa Kupima Madini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 18, 2018

NESCH MINTEC -Wachimbaji Tumieni Maabara za Kisasa Kupima Madini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED ambao ni wataalam wa madini aina zote katika mkutano wao na wadau wa Madini Kanda ya Ziwa uliofanyika  Jijini Mwanza,akieleza jambo.
Wito umetolewa kwa wachimbaji na wafanya biashara ya madini aina ya dhahabu kujenga tabia ya kutumia Maabara za Kisasa kupima madini hayo kabla ya kuyauza ili kuepuka upoteaji.
 

 Mkurugenzi wa NESCH MINTEC Bw.Happines Nesvinga amesema kuwa wachimbaji wa madini wamekuwa wakiendesha shughuli zao kienyeji hali inayowakosesha mapato na kupeleka kufanya kazi kwa hasara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED ambao ni wataalam wa madini aina zote katika mkutano wao na wadau wa Madini Kanda ya Ziwa uliofanyika  Jijini Mwanza,akieleza Namna bora ya kutumia Maabara za Kisasa kupima Madini kwa Wachimbaji wa Madini.

Wadau wakati wa Mkutano huo ambapo Baadhi ya Wachimbaji walioshiriki  akiwemo Mzee Cosmas Nkayamba mchimbaji wa dhahabu katika kata ya Nyakahula wilayani Biharamulo mkoani Kagera ,ammekiri kuwa uchimbaji wa kienyeji unawapa hasara na kuiomba Serikali kuwapatia elimu ili kuboresha shughuli zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad