DC Muleba Aagiza Kukamatwa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kitongoji kwa Kula Fedha za Wananchi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 19, 2018

DC Muleba Aagiza Kukamatwa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kitongoji kwa Kula Fedha za Wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango ameagiza wakamatwe Kaimu Mtendaji wa Kata ya Kyebitembe Bw. Jovin Ikongora pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kalinzi Bw. Asimwe Kishota kwa kosa la kula fedha za Wananchi shilingi laki Nne na Nusu.
Akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika April 17,2018  jioni kwenye kitongoji cha Kamshenyera kilichopo kijiji cha Bihata baaada ya Wananchi kutoa kero zao mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo, kuwa kaimu mtendaji wa kata alikula fedha shilingi laki tatu na Mwenyekiti wa kitongoji alikula shilingi laki moja na nusu ambazo fedha hizo zinatokana na kodi za wananchi hao. 

Mhandisi Ruyango amesema kuwa kutokana na tuhuma hizo zinazowakabili ni wajibu wa kuwafikisha mahakamani ili liwefundisho kwa watumishi wengine wanaohujumu fedha za wananchi na kuwataka viongozi wa vijiji na kata kutumia fedha kadri zilivyo changwa ili kuwaletea maendeleo ya wananchi hao.


Na Shafiru Yusuf-MULEBA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad