Yanga SC Usoni mwa Welayta Dicha F.C Kombe la Shirikisho. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 21, 2018

Yanga SC Usoni mwa Welayta Dicha F.C Kombe la Shirikisho.

Jinsi zitakavyokuwa mechi zote za mtoani Kombe la Shirikisho Africa.

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC wamepangwa kukutana na timu ya Welayta Dicha F.C (Wolaitta Dicha SC) ya Ethiopia katika hatua ya mtoano, kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Hiyo ni kwa mujibu wa droo iliyofanyika usiku wa leo March 21,2018 katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jijini Cairo, Misri ambapo Yanga itaanzia nyumbani kati ya tarehe 6, 7 au 8 mwezi Aprili na marudiano ni kati ya tarehe 17 au 18 mwezi Aprili mwaka huu.

Wapinzani hao wa Yanga SC wanaonekana kuwa ni miongoni mwa timu change barani Afrika, ikiwa imeanzishwa mwaka 2009, imefikia hatua hiyo baada ya kuitupa nje moja kati ya timu vigogo barani Afrika, Zamalek ya Misri kwa penati 4-3 baada ya kutoka sare ya jumla ya mabao 2-2.

Kwa upande wa vijana hao wa Jangwani wameingia kwenye hatua hiyo  baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1 iliyofungwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya sare 0-0 kwenye mchezo wa marudiano na wenyeji, Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.

Welayta Dicha imefika hatua hii baada ya kuitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 3-3, kila timu ikishinda 2-1 nyumbani kwake.

Katika Raundi ya Awali ambayo Yanga SC iliitoa Saint Louis Suns United ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Dar es Salaam na sare ya 1-1 Mahe, Welayta Dicha iliitoa Zimamoto ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Uwanja wa Amaan, kabla ya kushinda 1-0 Erthiopia.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo, Yanga inaangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mara ya nne kwa ujumla kihiostoria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad