Akitoa
mahubiri ya neno la Mungu Mzee wa kanisa
hilo Maila Mugeta alisema, mkono wa
Mungu uendelee kuwabariki na kuwatia
baraka wasimamizi wanaolea watoto hao,
wakijaliwa moyo wa huruma, kufundisha upendo na imani za kiroho.
Mugeta alisema watoto hao wanahitaji chakula na huduma nyinginezo wakati
wakifundishwa elimu ya dunia kupata ujuzi wa kitaaluma kupitia fani mbalimbali,
wakielekezwa kumfuata kristu kufundishwa maadili mema mbele za Mungu.
|
Aidha mkuu
wa kituo cha Nazaleti wilayani Ngara Francisca Bazimenyela amesema watoto
wanaolelewa kituoni hapo wanafikia 30 kati yao wapo waliofiwa na Wazazi na
wengine kutelekezwa kutokana na migogoro ya ndoa na kifamilia.
“Watoto hawa
walikosa malezi na elimu hivyo tunawapatia maadili ya kijamii na kiroho
changamoto kubwa ni kupungua wafadhili na hatuna shamba la kutuwzesha kulima
mazao ya chakula na bustani ya
mbogamboga”.Alisema Francisca.
|
Mmoja wa
waumini wa kanisa hilo Masumbuko Bwire amesema kanisa la Sabato Ngara mjini pia
limetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la Ngara ikiwa ni
utekelezaji wa wiki ya huruma kumuenzi
Kristu aliyefia msalabani
Bwire
alisema katika kipindi hiki cha Kwaresma waumini wanatafakari mafundisho ya
Kristo wakati alipokuwa akiwataja watu wenye shida na kuwahudumia kama
walemavu, wasioona na watoto waliomkimbila.
Pia Waumini
hao wametembelea Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara kutoa msaada wa damu kwa
ajili ya wagonjwa hasa watoto wachanga, wajawazito wanaojifungua kwa upasuaji
na wanaopata ajali za matukio mbalimbali.
|
No comments:
Post a Comment