Ahmed
anatoka katika kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromo ambalo limekuwa
likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015.
Daktari Abiy
Ahmed Ali, anayetoka jamii ya Oromo yenye watu wengi Ethiopia, amechaguliwa
kuwa mwenyekiti wa muungano unaotawala EPRDF, hatua itakayomfanya kuwa Waziri
Mkuu mteule wa nchi hiyo.
Ahmed
alichaguliwa kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa vyombo
vya habari vya serikali na atachukua wadhifa huo kutoka kwa Hailemariam
Desalegn aliyetangaza ghafla kujiuzulu mwezi uliopita.
Taifa hilo
kwa sasa liko katika hali ya dharura iliyotangazwa kwa ajili ya kumaliza
maandamano ya takriban miaka mitatu dhidi ya serikali.
Dkt Ahmed,
42, anatazamwa na wengi kama mwenye kuzungumza kwa uwazi, mwenye ujuzi na
uzoefu, na mwenye kukumbatia uongozi wa kuwashirikisha wote.
Anaaminika
kuwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana wa Kioromo na pia katika jamii
nyingine.
Wakosoaji
wake hata hivyo wanasema ni mtu wa ndani katika chama na hivyo basi, hakuna
matumaini ya kutekelezwa kwa matakwa ambayo yamekuwa yakiitishwa na
waandamanaji.
Ahmed
anatoka katika kabila kubwa zaidi nchini Ethiopia la Oromo ambalo limekuwa
likifanya maandamano ya kuipinga serikali tangu mwaka 2015.
Majuzi,
alichaguliwa mwenyekiti wa chama cha Oromo People's Democratic Organisation
(OPDO).
Miaka ya
nyuma aliwahi kuhudumu kama waziri na alikuwa na mchango mkubwa katika
kuanzisha shirika la ujasusi la taifa hilo.
Wakosoaji
wake hata hivyo wameelezea hofu zao juu ya ikiwa atapewa nafasi na mamlaka ya
kutekeleza mageuzi yaliyodaiwa na waandamanaji.
(Chanzo:BBC)
|
No comments:
Post a Comment