Mawasiliano ya Barabara ya Tabora hadi Itigi yakatika Baada ya Mvua Kubwa kunyesha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 22, 2018

Mawasiliano ya Barabara ya Tabora hadi Itigi yakatika Baada ya Mvua Kubwa kunyesha.

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Jana March 21,2018 katika eneo la Nyahua wilayani Uyui Mkoani Tabora imesababisha kukatika kwa barabara kuu ya Tabora kupitia Itigi hadi Dodoma na kusababisha magari ya abiria na mizigo kwishindwa kuendelea na safari zake kwa kutumia barabara hiyo.

Eneo la barabara lilikatika liko umbali wa Kilometa 79 kutoka Tabora Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio Meneja wa Wakala wa Barabara )TANROADS) Mkoa wa Tabora  Mhandisi Damian Ndabalinze alisema mvua zilizonyesha katika maeneo hayo zimesababisha kukatika kwa eneo hilo ambapo ndipo barabara ya lami inaishia.

Aliwataka madereva wa magari ya aina yoyote kuwa na subira kwa kutopita katika eneo hilo kwa sababu wanaweza kuhatarisha maisha yao na abiria na mizigo.

Alisema wakati taratibu nyingine zikiendelea za kutaka kurejesha mawasiliano kwa kutumia barabara hiyo ni vema magari yote ya kuja na kutoka Tabora yakapitia barabara ya Manyoni , Singida , Nzega hadi Tabora.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian  Kamuhanda alisema wamejipanga kutoka matangazo katika Stendi kuu ya mabasi Tabora na kushirikiana na Kikosi ya Usalama Barabara cha Mkoa wa Singida ili kuwaelekeza madereva wote wapiti njia ya Nzega ili kuepuka usumbufu.

Kwa upande wa Mtendaji wa Kata ya Kizenge Maganga Saulo alisema mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo ilikuwa kubwa na kusababisha kukatika kwa eneo hilo , hatua iliyopelekea magari kushindwa kupita.

Alisema ili kuhakikisha hakuna maafa yatakayotokea wanatumia Jeshi la Akiba kuwazuia madereva wanaotaka kujaribu kuvuka.
Baadhi ya wasafiri kutoka katika Basi la Prince Ramigo na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakijaribu kuvuka Jana March 21,2018 katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince  Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad